• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TIMU YA MPIRA WA WAVU (VOLLEYBALL) MKALAPA YAPONGEZWA

Posted on: August 31st, 2018

 Kuwa mshindi wa kwanza Kitaifa katika  mashindano ya UMITASHUMTA yaliyofanyika Jijini Mwanza mwezi huu mwaka huu 2018  kwa timu ya wasichana ya mpira wa wavu (Volleyball)  kutoka shule ya Msingi Mkalapa iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara yatupe funzo  viongozi, wazazi walezi na jamii kwa ujumla kuwa hakuna kinachoshindikana kama nia ya kufanya itakuwepo.

Timu ya volleyball wasichana shule ya masingi Mkalapa wakionesha mchezo wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza kwa kuwa washindi wa kwanza kitaifa mashindano ya UMITASHUMTA 2018 iliyofanyika shuleni  hapo

Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa Kamati ya Elimu Afya na maji ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mhe Chiputula Ibrahim katika sherehe ya kuipongeza timu hiyo kwa kushika nafasi ya kwanza  kitaifa katika mashindano ya UMITASHUMTA kwa mwaka huu na kueleza kuwa ushindi huo umeipa sheshima shule, jamii ya mkalapa hasa wazazi na walezi wa watoto, Halmashauri, Mkoa na Taifa kwa ujumla  kwa viwango vyao vya uchezaji hivyo wananastaili pongezi za dhati kabisa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu Afya na maji ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mhe Chiputula Ibrahim akihutubia wananchi na wananfunzi wakati wa hafla fupi ya kuwapongeza kwa kuwa washindi wa kwanza kitaifa mashindano ya UMITASHUMTA 2018 iliyofanyika shuleni  hapo

Chiputula aliendelea kueleza kuwa kuna baadhi ya wazazi wameendelea kuwa na dhana potofu kuwa michezo ni uhuni au kupoteza muda lakini kwa sasa dunia imebadilika michezo ni ajira, inaongeza chachu ya wanafunzi kupenda shule, ni afya lakini pia inampa fursa mwanafunzi kuongeza jografia kwa kukutana na watu tofatu katika mazingira mengine tofauti na nyumbani mambo ambayo yatamsaidia katika maisha yake ya baadae.

Timu ya wasichana 9 ya mpira wa volleyball iliyoshiriki michezo ya UMITASHUMTA  mwaka 2018 na kuwa washindi wa kwanza kitaifa kati yao sita wako darasa la saba katika hafla fupi ya kuwaongeza kwa ushindi huo

“Timu hii inaundwa na wasichana 9 walioshiriki mashindano haya, leo tunawapongeza kwa kuwapata zawadi mbalimbali, tukio la leo liwape chachu wazazi wengine kuwaruhusu watoto wao kushiriki kwenye mazoezi ya michezo mbalimbali ili kuwapa fursa ya kujifunza maana michezo ni sehemu ya masomo ambayo wakiyazingatia yatawasaidia kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa” alisisitiza Chiputula.

Wananchi na wananfunzi wakiwa kwenye  hafla fupi ya kuipongeza timu ya volleyball iliyopata ushindi wa kwanza kitaifa

kwa upande wake Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri hiyo Elizabeth Mlaponi alisema kuwa timu hiyo imekuwa ikicheza vizuri kwa muda sasa lakini kadri miaka inavyoenda kinafanya vizuri zaidi kutokana na juhudi anazozifanya Kocha wa mchezo huo ndugu Gabriel Joshua  ambaye anajitolea kuwafunsisha wanafunzi, kama Halmashauri tunampongeza sana maana yeye ndio chanzo cha ushindi huu.

Kocha wa timu ya volleyball kituo cha Mkalapa Gabriel Joshua akipeana mkono na Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Elizabeth Mlaponi  baada ya kupokea zawadi kwenye  hafla fupi ya kuiwapongeza timu ya wasichana iliyopata ushindi wa kwanza kitaifa katika mashindano ya UMITASHUMTA 2018

Aidha Afisa elimu amewaasa wazazi wote kuto katisha ndoto za watoto wao kwa kuwawambia wafanye vibaya kwenye mitihani yao ya kumaliza elimu  ya msingi ambayo itafanyika mwanzoni mwa mwezi wa tisa maana tabia hiyo inafanywa na baadhi ya wazai kwa maslahi yao binafsi jambo ambalo linawanyima watoto haki ya kupata elimu.

Afisa Elimu Msingi Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Elizabeth Mlaponi akitoa neno kwenye hafla fupi ya kuiwapongeza timu ya wasichana iliyopata ushindi wa kwanza kitaifa katika mashindano ya UMITASHUMTA 2018

Mlaponi amewaasa wazazi wenye tabia ya kuwashawishi wanafunzi kutofanya vizuri mitihani yao ya kumaliza elimu ya msing  kwa kusema  kuwa “kwa maisha ya sasa elimu ni kila kitu hata kwenye michezo elimu pia inatakiwa hivyo waachenoi watoto wafanye mitihani yao vizuri ili waendelee na elimu ya sekondari kwani serikali inatoa elimu bila malipo hivyo acheni tabia hiyo inarudisha nyuma maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla”

Kwaya ya wanafunzi wa shule ya masingi Mkalapa wakitumbuiza wakati wa hafla fupi ya kuiwapongeza wanafunzi wenzao walioshiriki mchezo wa volleball na kuwa washindi wa Kwanza kitaifa


Akizungumza kwa niaba ya wazazi wa watoto walioshiriki mashindano hayo bibi Amina Lukas alieleza kuwa amejisikia vizuri mtoto wake kuwa sehemu ya ushindi huo, lakini pamoja na kushinda  mtoto wake  pia amekuwa na nidhamu, anajituma katika masomo maana michezo inamwongezea umakini katika kufanya kila jambo.

Walimu wa shule ya masingi Mkalapa wakiwa kwenye halfa ya kuwapongeza wanafunzi wao kwa ushindi waliopata.

“Namshukuru mwalimu anayewafundisha kwa kweli anawasaidia watoto na mimi kama mzazi namuruhusu kila siku kwenda kwenye mazoezi lakini pia namshauri kuzingatia masomo darasasni kwani michezo inaenda sambamba na kufanya vizuri kwenye masomo” alisema Amina.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • MSIGWA: MAAFISA HABARI NI SAUTI YA SERIKALI, TANGAZENI MAFANIKIO YA SERIKALI KWENYE MAENEO YENU.

    May 25, 2025
  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI MNAKUWA WABUNIFU NA WAZALENDO ILI WANANCHI WAPATE HABARI SAHIHI NA KWA WAKATI.

    May 23, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MASASI DC KWA KISHINDO:WATEMBELEA MIRADI MITANO YENYE THAMANI YA TSH.MILIONI 678,844,040.00

    May 19, 2025
  • WATENDAJI WA SERIKALI TEKELEZENI WAJIBU WENU WA KIKAZI,MSIJIHUSISHE NA MAMBO YA SIASA: BARAZA LA MADIWANI

    May 15, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa