Tatizo la wananchi wengi wa kata zilizopo pembezoni mwa mto Ruvuma katika halamashauri ya wilaya ya masasi kupoteza maisha au kuata ulemavu wa kudumu kutokana na mamba wanaopatikana katika mto huo linatarajiwa kuisha kabisa baada ya mradi wa maji unaotekelezwa kutokana na chanzo mto huo kukamilika.
Kauli hiyo imetolewa na Mhadisi wa maji wa halmashauri hiyo Mhandisi Francis Bwire wakati wa akikagua utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya shilingi bilioni 2.7 ambao unatarajia kusambaza maji katika vijiji 8 vyenye jumla ya watu 17420 ndani ya kata ya chikolopola na Mnavira.
Bwire alisema kuwa wananchi wa kata hizo kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitegemea mto Ruvuma kupata huduma ya maji kwa matumizi mbalimbali hali ambayo imekuwa ikipelekea wananchi wengi kujeruhiwa au kuuawa na mamba wakati wa kuchota maji na shughuli zingine, hivyo mradi huu utaondoa kabisa tatizo hili kwa kuwa wananchi watapata huduma ya maji katika maeneo yao na sio kuja mtoni tena.
“watu wengi wamepoteza maisha huku wengine wakipata ulemavu wa kudumu uliosababishwa na mamba wanaopatikana katika mto Ruvuma” alisema Bwire.
Bwire alisema kuwa utelezaji wa mradi huo hadi sasa upo asilimia 70 ambapo ujenzi wa matenki mawili yenye ujazo wa lita 100,000,ukarabati wa tanki 1 lenye ujazo wa lita 25,000, ujenzi wa vituo 38 vya kuchotea maji, ulazaji wa bomba kubwa kilomita 12 na ndogo kilomita 9 umekamilika na ujenzi wa chanzo unaendelea.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa