Tarehe 1 Oktoba ya kila mwaka, ni kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani iliyoanzishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 14 Desemba 1990. Maadhimisho haya ni sehemu ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Vienna wa Mwaka 1982 kwa Ajili ya Wazee Duniani, “The Vienna International Plan of Action on Ageing” ulioboreshwa tena na Mkakati wa Madrid, Hispania wa Mwaka 2002 ili kuweza kupambana na changamoto za wazee katika Karne ya 21 na kuendelea mchakato wa maendeleo fungamani ya binadamu kwa ajili ya wote. Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani ni moja kati ya jitihada za Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) katika kutambua na kuhamasisha jamii kuweza kulinda na kutetea haki msingi za wazee duniani. Maadhimisho ya Mwaka 2021 yananogeshwa na kauli mbiu “Matumizi Sahihi ya Kidigitali kwa Ustawi wa Rika Zote.”
Mh.Mariam Chaurembo (Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu) ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo ya Siku ya Wazee Duniani akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gagut yaliyofanyika Leo tarehe 01.10.2021 ambapo Kimkoa yaliadhimishwa katika kijiji cha Nagaga kilichopo katika kata ya Lulindi Halmashauri ya Wilaya ya Masasi akiongea na Wazee hao alisema, kwa sasa kuna ongezeko kubwa la wazee Duniani jambo ambalo limezidisha changamoto nyingi kwa wazee kama vile mauaji kwa wazee yatokanayo na imani za kishirikina katika Maeneo mbalimbali,kutokwepo kwa huduma bora za kiafaya,Kipato Duni, Kuachiwa mzigo Mkubwa wa kulea watoto Yatima, Aliendelea kusema kwa kuziasa Halmashauri zote ndani ya Mkoa kuwa kuanzia Novemba 30 Mwaka huu kuchukua hatua mbalimbali ili kuwasaidia wazee ikiwemo kuanzishwa kwa Mabaraza ya Wazee ya katika ngazi zote , kubaini wazee wote wenye mahitaji Maalumu na kuwapatia kadi za Bima ya Afya ili waweze kupatiwa Matibabu bila malipo
Hii ni siku ambayo imetumika pia kwa ajili ya maboresho ya afya ya wazee sehemu mbalimbali za dunia, kwa kuwapima magonjwa kama vile: Kisukari, BP, Tezi Dume pamoja na kupatiwa huduma za msaada wa kisaikolojia sanjari na elimu ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19. Bado kuna haja ya kuendelea kuboresha huduma ya afya, elimu, lishe, kipato na makazi kwa wazee wengi, ili waweze kuishi kwa amani, furaha na utulivu na kuwaasa Wazee wote kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kupata chanjo ya Uviko-19 katika maeneo mbalimbali ya Vituo vya kutolea huduma.
Lakini pia alitumia siku ya leo Mbele ya Wazee hao kwa kuwataka Kujiandaa kwa ajili ya Ujio wa Zoezi la Sensa ya Watu na Makazi, zoezi ambalo linategemewa kuanza Mwakani Mwezi oktoba 2022, japo Maandalizi yake yanategemewa kuanza hivi karibuni kwa kufanya Sensa ya Majaribio katika Baazi ya Maeneo nchini Mwisho aliwashukuru Wazee wote kwa kuendelea kutoa Michango yao kwa kuendelea kujijenga kiuchumi na kuujenga uchumi wa taifa kwa ujumla .
Kaimu Mkurugenzi wa Halamshauri ya Wilaya ya Masasi Ndugu Joshua Sanga (Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya Masasi) akiwakaribisha Wageni wake Kutoka Maeneo Mbalimbali wakiwemo Wazee leo tarehe 01.10.2021 katika Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani ambapo Kimkoa Sherehe hizi Zimefanyika katika Kijiji cha Nagaga Halmashauri ya Wilaya ya Masasi yenye Kauli Mbiu “Matumizi Sahihi ya Kidigitali kwa Ustawi wa Rika Zote.” ambapo pia Kaimu Mkurugenzi alichukuwa nafassi hii kuwaasa Wazee na Vijana Kujitokeza kwa wingi Kushiriki kwenye Zoezi la Chanjo ya Uviko-19 Katika Vituo vyetu mbalimbali vya Kutolea huduma.
Mratibu wa Chanjo wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Bi.Brandina Mpunga akiwa amesimama mbele ya Wazee akiwaasa juu ya kupatiwa Chanjo ya Uviko-19 akitumia fursa hiyo pia kwa kutoa Elimu kwa Wazee hao juu ya Umuhimu wa kuchanja na kuondokana na Imani potofu zinazoenezwa Mitaani juu ya Chanjo hizo, ambapo kwa siku ya leo ambayo ni Uzinduzi wa chanjo awamu ya Pili Muitikio kwa Wananchi Umeonekana kuwa Mkubwa sana katika Maeneo mbalimbali ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
Daktari akiwa na mmoja kati ya Wazee walio hudhulia kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani akitoa huduma ya Vipimo bure kwa wazee hao kwa magonjwa kama vile: Kisukari, BP, Tezi Dume pamoja na kupatiwa huduma za msaada wa kisaikolojia sanjari na elimu ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19.
Kikundi cha Sanaa za Ngoma za Asili kikitumbuiza mbele ya Wazee, pamoja na Meza Kuu kwa kutoa Burudani mbalimbali wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani ambayo hufanyika kila Mwaka tarehe moja Mwezi Oktoba yenye Kauri mbiu Mwaka huu “Matumizi Sahihi ya Kidigitali kwa Ustawi wa Rika Zote.”
Muguzi wa Afya akiendelea na Zoezi la Kutoa Chanjo ya UVIKO-19 kwa Wazee Waliojitokeza leo tarehe 01.10.2021 katika kuadhimisha Siku ya Wazee Duniani ambapo Kimkoa ilifanyika Katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Katika KIjiji cha Nagaga
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa