• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Serikali Wilayani Masasi yawashika mkono Wananchi Mtengula waliopatwa na maafa ya mvua.

Posted on: May 9th, 2024

Serikali Wilayani Masasi leo tarehe 08/05/2024 imetoa bati 86, boriti 97, misumari kg 40, saruji mifuko 10, na chakula  kwa familia zilizopatwa na maafa ya mvua iliyoambatana na upepo mkali na kusababisha baadhi ya  familia kukosa makazi, mvua iliyonyesha siku ya tarehe 01/01/ 2024 majira ya saa 2:00 usiku.

Tukio hilo limetokea Katika Kijiji Cha Mtengula, kata ya Mijelejele Halmashauri ya Wilaya Masasi Mkoani Mtwara.

Akigawa vifaa hivyo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe.Lauter Kanoni, Afisa Tarafa ya Chiungutwa  Bw. Ali Kuchele amesema kwamba kufuatia tathimini iliyofanywa na timu ya Wataalamu Kutoka ngazi ya Halmashauri ilibaini uwepo wa uharibifu wa aina mbili, kwanza uharibifu wa makazi, na uharibifu maeneo ya biashara ambapo  katika Eneo la Mijelejele walipatikana watu 17 na katika Kata ya Chiungutwa zilipatikana kaya 146, lakini kwavile kilichopatikana hakiwezi kuwatosheleza watu wote,na ndipo wakaamua kwa kuanzia wapewe kipaunbele wale wote ambao wamekosa makazi moja kwa Moja na wapo katika hali mbaya zaidi.


Amesema "mnamo Siku ya tarehe 01/01/2024 katika eneo la Wilaya yetu ya Masasi ilijitokeza maafa ya mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali na maeneo yaliyokuwa yameathirika zaidi ni mawili kata ya Mijelejele na Kata ya Chiungutwa ambapo kwa jitihada kubwa zilizofanywa na Mkuu wa Wilaya ya Masasi kuwatafuta wadau mbalimbali ili kuweza kupata chochote kitu (msaada) ili kuwashika mkono ndugu zetu na baada ya hapo mkuu wa Wilaya aliweza kufanya Uzinduzi wa ugawaji wa vifaa hivyo katika Tarafa ya Chiungutwa kwani jumla ya shilingi milioni 22,600,000 zimetolewa kwaajili ya kuwashika mkono waathirika hao"...... alisema Bw. Kuchele.

Ameongeza kuwa" Mkuu wa Wilaya ametoa salamu hizi za pole kwenu na pia anawashukuru kwa ustahamilivu wenu tangu mlipopata maafa hayo na pia tunawashukuru sana watu wengine pamoja na ndugu zenu kwa kuwapa msaada wa makazi kwa muda."

Naye Diwani wa kata hiyo ya Mijelejele mhe. Juma Pole pamoja na kuendelea kuwapa pole kwa maafa hayo pia ametumia nafasi hiyo kuwaeleza wananchi hao kuwa, Serikali ya awamu ya 6 inawapenda sana kwasababu maafa hayo ya tarehe mosi hayajaigusa Mijelejele peke yake bali ni maafa ambayo yametokea maeneo mengi katika Eneo la Masasi, katika Mkoa na Tanzania kwa ujumla hivyo yawapasa  kumuombea dua njema mhe. mkuu wa Wilaya ya Masasi Lauter Kanoni kwa kazi kubwa ambayo anaifanya kwenye Wilaya ya Masasi sanjari na msaada huu ambao Leo wana Mijelejele wameupata.

Amesema vifaa hivi hawawezi kupata watu wote isipokuwa wanatakiwa kushukuru kwa kile walichokipata kwani Serikali haiwezi kumaliza kila kitu bali inakuja kuchochea pale ambapo wao wanapaswa waanze kufanya.


Mzee chifu Magambo pamoja Naye  Bw. Ali Bakari ambaye ni Imamu wa msikiti wa Mtengula, Hawa ni miongoni mwa walengwa waliopata msaada huo wote kwa Pamoja wamewashukuru viongozi wote ambao wameungana na kufanikisha wao kupatiwa misaada hiyo ambayo ilikuwa ikifanyika katika maeneo mengine Lakini Leo na wao wamepatiwa .


Imeandaliwa na Winifrida Ndunguru,

...............Afisa Habari MDC

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO ROBO YA III (JAN -MACHI 2025) INAYOTEKELEZWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI.

    May 06, 2025
  • PPRA YATOA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO WA NeST NA SHERIA YA UNUNUZI WA UMMA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI

    March 12, 2025
  • KAMATI YA SIASA YA CCM WILAYA YA MASASI YAFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI.

    March 06, 2025
  • MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI YANATOA FURSA KILA MMOJA KUJUA HAKI YAKE YA MSINGI: MHE MAJALIWA

    March 06, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa