Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya kusini imeamua kuwajengea uwezo viongozi wanawake wa ngazi mbalimbali wakiwemo madiwani na wakuu wa idara katika wilaya 5 na Halmashauri 7 za Mkoani Mtwara lengo ikiwa ni kuwaongezea uelewa kuhusu maadili ya viongozi wa umma katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika tarehe 21 setemba 2018 wilayani Masasi, Katibu Msaidizi Ofisi ya Rais Maadili ya Viongozi Kanda ya Kusini ndugu Mayina Henjewele alisema kuwa mafunzo hayo yatatoa fursa kwa viongozi hao kujua majukumu na wajibu wa sekretarieti ya maadili pamoja na mambo muhimu ya kuzingatia katika utumishi wa umma ikiwemo sheria na kanuni
Mwezeshaji kutoka ofisi ya maadili Mtwara ndugu Ramadhani Ramadhani akitoa mafunzo kwa viongozi wanawake mkoa wa Mtwara yaliyofanyika wilayani masasi
Henjewele alifafanua sababu za mafunzo hayo kuwa ni baada ya kufanyika utafiti mwaka 2015 kupitia taasisi yao ya kukuza uelewa kwa wananchi kuhusu majukumu ya sekretarieti hiyo ambapo ushiriki wa wananwake katika kutoa taarifa za ukiukwaji wa maadili kwa viongozi wa umma ulikuwa mdogo sana ukilinganisha na wanaume.
“Matokeo yalionesha kuwa asilimia moja tu ya wananwake katika maeneo ya vijiji na miji walioweza kutoa taarifa za ukiukwaji wa maadili miongoni mwa viongozi wa umma”
Alisema hali hiyo ililazimu Sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma kuandaa mafunzo hayo katika mikoa yote inayotekelezwa mradi huo ikiwemo Mtwara. "Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uelewa viongozi wanawake katika mamlaka za Serikali za mitaa kuhusu maadili ya viongozi wa umma ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia maadili.
Aidha, Henjewele alisema kuwa viongozi wananwake kuna wakati wanashindwa kutekeleza majukumu yao kama viongozi kwa kuwa hawana uelewa wa mambo mbaimbali ya kimaadili “tunawajengea uwezo wa kujiamini kwa kujua sheria na taratibu lakini pia kufahamu wajibu wao kama viongozi katika kutumikia wananchi”
Mwezeshaji kutoka ofisi ya madili ndugu Irene Triplow akitoa mafunzo kwa viongozi wanawake mkoa wa Mtwara yaliyofanyika wilayani masasi
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya masasi Emmanuel Ryoba wakati akifungua mafunzo hayo, aliwaeleza viongozi hao kusikiliza kwa makini mafunzo hayo ili baada ya kupata mafunzo hayo i wakawahamasishe na kuwaelimisha wanawake wengine katika ngazi za chini kwenye mitaa na Kata itanisaidia kuwajengea ujasiri wa kutoa taarifa kwenye mamlaka husika pindi wanapokumbana na ukiukwaji wa maadili
Ryoba aliwakumbusha viongozi hao kuwa Wananchi wanawategemea hivyo ni vema wakatumia nafasi zao kuleta maendeleo ikiwemo kuelimisha wananchi juu ya mambo mbalimbali, ni lazima wawe mfano wa kuigwa, kwa kuwa wawazi na kuwajibika ipasavyo pamoja na kuzingatia ahadi za uadilifu walizoapa baada ya kupata dhamana hizo.
Akiongea kwa niaba ya madiwani wenzake mhe. Asha Rashid Tebwa diwani wa viti maalum kata ya milongodi wilaya ya Tandahimba alisema kuwa “Mafunzo ni mazuri yatatusaidia katika utendaji kazi wetu ikiwemo kufuata sheria na taratibu lakini Elimu ya maadili inapaswa ipelekwe kwenye ngazi ya vijiji na kata maana huko ndiko kwenye wananchi wengi”
Mhe. diwani Asha Rashid Tebwa diwani wa viti maalum kata ya milongodi wilaya ya Tandahimba akichangia hoja wakati wa mafunzo
Mhe Asha amewashauri wanawake wenye ndoto za kuwa viongozi lazima wafahamu sheria na taratibu za kuwa viongozi bora, lakini pia wajiamini kutoa maoni katika vikao mbalimbali vya maamuzi na kutetea hoja zao badala ya kuwaachia wanaume waamue badala yao. “Hakuna aliezaliwa kiongozi Uongozi ni kujifunza”
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa