Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe.Dkt Medard M. Kalemani (MB) azindua rasmi Mradi wa umeme vijijini (REA) awamu ya tatu katika Mkoa wa Mtwara tarehe 17.08.2017 ambapo vijiji 213 mkoani mtwara vitapata umeme kupitia mradi huu.
Uzinduzi huo kimkoa umefanyika katika Wilaya ya Nanyumbu katika kijiji cha Mnazimmoja kilichopo eneo la Michiga na kusema kuwa, serikali imedhamiria kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya umeme ili waweze kuufikia uchumi wa viwanda ambayo ndio azima ya serikali .
Dkt kalemani amewaeleza wananchi kuwa mradi huo wa umeme utasukuma kwa kasi ya safari ya kuufikia uchumi wa kati kupitia viwanda ambapo wananchi wa mtwara na vijiji vyake watapata fursa ya kufungua viwanda vidogo na vikubwa na hivyo kuongeza uzalishaji wa bidhaa na kukuza uchumi.
Naibu waziri amesema kuwa, Mtwara ni kati ya mikoa mitano ya Tanzania bara ikiwemo Lindi, Rukwa Katavi na Kigoma iliyokuwa nyuma katika huduma ya umeme hivyo serikali imeamua kutatua changamoto hiyo kwa vitendo kwa kuanzia mkoa wa mtwara wenye rasilimali ya Gesi.
“katika awamu ya kwanza na ya pili ya mradi wa REA Mkoa wa mtwara ulifanikiwa kupata viiji 82 ambapo awamu ya kwanza vijiji 31 tu ndio vilipata umeme na awamu ya pili vijiji 5, lakini awamu ya tatu vijiji 283 vimeingizwa kwenye Mradi, lengo la serikali ni kuiniza vijiji vyote vilivyobaki” alifafanua Dkt kalemani.
Naibu waziri alisema kuwa katika mradi huo wa umeme vijijini awamu ya tatu taasisi mbalimbali zikiwemo mashule, zahanati makanisa na misikiti na makanisa bure ili kuboresha upatikanaji wa huduma kwa urahisi zaidi.
Naibu waziri amewaelekeza wakandarasi waliopata kazi hiyo kuhakikisha wanaweka umeme kila kijiji,kitongoji na nyumba bila kujali aina ya nyumba, wametakiwa kutumia nguvu kazi ya vijana waliopo Mtwara na mwalipe kwa wakati pamoja na kutekeleza mradi kwa muda wa miezi 24 kama mkataba unavyoelekeza.
Pamoja na uzinduzi huo mhe. Kalemani ametoa vifaa vya umeme 20 kwa wazee wa kijiji cha Mnazimoja ambao hawatakuwa na uwezo wa kufanya wiringi kwenye nyumba zao mara baada ya umeme kusambazwa kwenye maeneo yao
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa