Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa kupata HATI SAFI baada ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2019 kutoa taarifa ya matumizi ya fedha ya halmashauri hiyo kuwa yamefuata taratibu na sheria ya matumizi ya fedha za serikali.
Pongezi hizo amezitoa jana tarehe 03 Juni, 2020 kwenye baraza maalumu la madiwani la kupitia taarifa ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali za halmashauri hiyo kwa mwaka wa fedha unaoishia 30 Juni, 2019 na kueleza kuwa "Halmashauri hii ni ya kwanza katika halmashauri Zangu 9 za mkoa wa Mtwara kwa kujibu vizuri hoja za mkaguzi hali iliyopelekea hoja zaidi ya 65% kufungwa, hongereni sana"
Aidha, Byakanwa ameendelea kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa kuweza kukusanya mapato kwa zaidi ya 100% ndani ya kipindi cha robo tatu ya mwaka wa fedha 2019/2020. Aidha "nawapongeza kwa kuanzisha shamba la ufuta na korosho ikiwa ni jitihada za halmashauri kuwa na vyanzo vya mapato vya uhakika badala ya kutegemea zao la korosho pekee"
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa