Kufuatia hatua iliyochukuliwa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Byakanwa kwa viongozi 56 wa Vyama vya ushirika wilayani Masasi kwa kuwaweka ndani tarehe 23 februari, 2018 kwa makosa ya kutowalipa wakulima wa korosho kama ilivyobainishwa kwenye ripoti ya uchunguzi jumla ya shilingi milioni 39, 450,000 zimesharejeshwa na viongozi Hao.
Hayo aliyasema wakati akiwasilisha taarifa ya Mkoa wa Mtwara mbele ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muunganno wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa katika viwanja vya Ikulu ndogo Mjini Masasi katika ziara yake ya kikazi ya kutembelea mkoa huo ambapo ameeleza kuwa baada ya kuona baadhi ya wakulima wa zao la korosho hawajaripwa fedha zao, mkoa uliamua kufanya uchunguzi kubaini nani anahusika na tatizo hilo na baada ya ripoti kutolewa ndipo viongozi hao wakabainika.
Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi iliyowasilishwa tarehe 23 februari, 2018 ilibainisha kuwa kwa msimu wa 2017/18, Tume ilikutana na jumla ya wakulima 1,290 wanaodai kilo 444,578 zenye thamani kati ya Shs. 1,533,794,100 na 1,803,208,368 kutegemea kwa mnada wa bei ya chini Shs. 3,450 na bei ya juu Shs. 4,056 wanaodai malipo ya korosho kwa baadhi ya minada kwa sababu mbalimbali iwemo Makatibu wakuu wa vyama vya ushirika kuchelewesha malipo ya wakulima bila sababu za msingi,
Pia sababu nyingine ni wakuu kulipa kilo pungufu na zile zilizopokelewa ghalani na Baadhi ya wakulima kupima korosho ghalani bila kufungua akaunti za benki kwani mfumo wa Benki ni mpya kwa wakulima na wakulima walio wengi hawana elimu ya matumizi ya Benki
Byananwa amemweleza Mhe Waziri Mkuu kuwa Mkoa utaendelea kuchukua hatua ili wakulima wapate haki yao.
Aidha Byakanwa pamoja na masuala ya korosho amewasilisha Tatizo la Mji na umeme kwa mkoa wa Mtwara hasa kwa wilaya ya Masasi
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa