Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan Sept 16, 2023 ameweka Jiwe la Msingi kwenye Jengo la Utawala la Halmshauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
Mradi huo ambao unatekelezwa kwa Force account kupitia kwa fundi Ujenzi Chuo kikuu cha Sayansi na Teknoloji Mbeya {MUST} na Mhandisi Mshauri Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam{ BICO}, ulianza utekelezwaji wake tarehe 6/4/2021 hadi sasa upo katika hatua ya umaliziaji umegharimu kiasi cha fedha shilingi bilioni 2.66 .
Hata hivyo baada ya zoezi hilo la uwekaji wa jiwe hilo la msingi katika jengo hilo la utawala, Rais Dkt Samia aliwasalimia Wananchi wa Lulindi ambao walijitokeza hapo kumlaki, ambapo aliwasisitiza kuongeza jitihada kwenye Kilimo na hasa cha Mbaazi, Korosho na Ufuta waongeze maeneo mengi Zaidi ya kulima na akawahaidi kuwa, Serikali nayo itajitahidi kutafuta masoko ya uhakika ili baada ya mavuno yao na kuuzwa zipatikane fedha nyingi ambazo zitamnufaisha mkulima mwenyewe moja kwa moja, nayo serikali itaendelea kuzipeleka fedha kwenye Halmshauri.
Amesema kwasasa Maendeleo yeyote ni fedha ambayo Serikal inakusanya kwenye kodi na ikishindikana kwenye kodi basi hujielekeza kwenye mikopo, na hivyo ili kuepuka suala la mikopo ni lazima Wananchi nao wakaisaidia Serikali kukusanya fedha za Maendeleo kwa kujikita kwenye shughuli za kilimo.
Hata hivyo Rais Samia ambaye alianza ziara yake mkoani Mtwara tarehe 14 Sept 2023, amehitimisha ziara yake jana 17 Sept 2023 kwa kuzungumza na Wananchi wa wilaya ya Masasi katika mkutano wa hadhara uliofanyika ktika uwanja wa bomani masasi mjini huku akiwashukuru Wananchi wote wa mkoa wa Mtwara kwa kujitokeza kwa wingi kumpokea na kuhudhhuria mikutano myake yote ya hadhara aliyoifanya katika Wilaya zote za Mkoa wa Mtwara.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa