Viongozi wa Halmashauri zote Mkoani Mtwara wamepewa mwezi mmoja kwaajili ya kutenga maeneo yatakayo jengwa vituo vya kuwezesha wananchi kiuchumi.
Agizo hilo amelitoa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala leo juni 25,2024 kwenye kikao cha viongozi kupewa uelewa wa programu ya uwezeshaji wananchi kiuchumi "IMARISHA UCHUMI NA SAMIA"(IMASA) inayoratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) kwenye ukumbi wa BOT uliopo Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara uliowakutanisha viongozi mbalimbali wa serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali.
Amesema kuwepo kwa vituo hivyo kutasaidia upatikanaji wa wananchi kwa urahisi pindi wanapotakiwaa kupewa elimu hivyo ameagiza kuwepo kwa vituo 10 katika mkoa wa Mtwara.
"Mkoa wetu bado hauna hata kituo kimoja cha uwezeshaji kwa wananchi wetu kiuchumi,ndani ya mwezi mmoja tuwe tumeshatenga maeneo hayo kila halmashauri natarajia kufikiabtarehe 30 mwezi wa 7 nisikie kuna vituo 10 kwamana halmashauri 9 na mkoa lazima tuwe nacho ili wananchi wetu tujue tunakutana nao wapi kwaajili ya mafunzo."
Aidha amewataka viongozi wote kwenda kutekeleza majukumu yao ipasavyo kama viasharia vinavyotakiwa na amewataka kupata maelekezo mahususi kutoka kwa wataalamu.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mtwara Saidi Nyengedi amesema program hiyo kama itatekelezwa kikamilifu itachochea ukuaji wa uchumi kwa taifa,hivyo amewaomba waratibu wote kwa ngazi ya mkoa na halmashauri kuratibu na kusimamia utekelezaji wake kwa uadilifu bila upendeleo.
Nae Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezesha Wananchi Kiuchumi (NEEC)Bengi Issa, amesema program ya wezesha wananchi kiuchumi inalenga kuwasaidia wananchi zaidi na kuimarisha kile ambacho mwananchi amekianzisha kwa kumboreshea mtu yoyote mwenye shughuri za kiuchumi ambapo wanufaika ni wanawake,vijana na makundi maalamu.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa