NAIBU KATIBU MKUU OR-TAMISEMI AIPONGEZA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI UPANUZI WA KITUO CHA AFYA NAGAGA.
“Wahenga walisema kilio lia na mwenyewe, mlilia, tukasikia, na kutokana na kilio chenu tukaja tulie pamoja na hatimaye zikaletwa fedha shilingi milioni 400 kwa ajili ya upanuzi wa kituo cha afya cha Nagaga na majengo yanaonekana, nawapongeza” alieleza Naibu Katibu Mkuu OR- TAMISEMI Dr. Zainabu Chaula wakati alipotembelea utekelezaji wa mradi wa upanuzi wa kituo cha afya Nagaga unaolenga kukifanya kituo hicho kutoa huduma bora kwa wananchi wa Kata ya Namalenga na vijiji jirani.
Dr. Chaula amesema, utekelezaji wa mradi huo umezingatia thamani ya fedha iliyotolewa kwani majengo ni mazuri na yana ubora unaotakiwa hivyo adhima ya serikali ya kuboresha miundombinu na huduma za jamii kwa ujumla inatekelezeka kwa vitendo baada ya kuona majengo ambayo yamejengwa katika kituo hicho cha Nagaga.
Pia Dr. Chaula amewapongeza wananchi wa Nagaga kwa ushirikiano wanaoutoa katika utekelezaji wa mradi huo na hivyo inaashiria wananchi kuwa wanatambua mipango ya serikali na kuiunga mkono kwani suala la maendeleo linahitaji ushirikiano kati ya serikali, wadau wa maendeleo na wananchi wenyewe na sio kuiachia serikali pekee.
Katika mradi huo jumla ya majengo matano ikiwemo jengo la maabara, upasuaji, wodi ya wazazi, jengo la kuhifadhia maiti na nyumba ya mtumishi kwa gharama ya shilingi milioni 400.
Aidha Dr Chaula amewaeleza wananchi kuwa, majengo hayo yamejengwa na mafundi wa kawaida kwa kushirikiana na wataalamu hivyo nawakumbusha vijana wenye ujuzi kujiunga kwenye vikundi ili waweze kupata fursa za kupata mikopo, kandarasi za ujenzi wa miradi na huduma mbalimbali kwani serikali imedhamiria kuwainua vijana kwa kuwapa fursa mbalimbali za kushiriki kwenye shughuli za maendeleo na kuwaongezea kipato.
Akizungumzia kwa niaba ya wananchi wa kijiji cha Nagaga ndugu Afati Mangochi alisema kuwa wananchi wanaipongeza serikali kwa kuleta fedha za kupanua kitu hiki cha afya ambacho kikikamilika kitasaidia utoaji wa huduma za uhakika kwa wananchi wa Nagaga na walio nje ya nagaga wapatao 129,609 sawa na 47% ya wakazi wote wa masasi.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Namalenga mhe. Arafath Ismail Hassani ameahidi kuendelea kusimamia miradi huo mpaka utakapokamilika pamoja na kuhamamsisha wananchi kujitolea kwa hali na mali kuunga mkono serikali katika kuboresha na kusogeza huduma za jamii kwa wananci ikiwemo usimamizi wa miradi inayotumia fedha za serikali na wadau wa maendeleo.
Halmashauri ya wilaya ya Masasi ina jumla ya vituo vya kutolea huduma ya afya 47 ambapo kati ya hivyo vituo vya afya ni 2, na zahanati 31 zinazomilikiwa na serikali vingine 14 vinamilikiwa na wadau wenngine kama dini na watu binafsi.
Nyumba ya mtumishi kituo cha Afya Nagaga
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa