Mwenge wa Uhuru 2024 leo june 5,2024 umeanza mbio zake Wilayani Masasi ambapo katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi tayari umekimbizwa umbali wa kilomita 102 kwa kupitia katika vijiji 22, kata 12 na Tarafa 2.
Aidha Mwenge wa uhuru kitaifa umepita katika miradi saba (7) ya maendeleo yenye thamani ya jumla ya shilingi bilioni mbili na milioni mia nane ishirini na tisa laki tisa na sabini elfu mia tatu ishirini na tano (2,829,907,325.00 kutoka katika sekta za Barabara, Afya, Maendeleo ya jamii, Elimu, Mazingira na huduma za kukuza uchumi.
Kati ya miradi hiyo, miradi miwili (2) imezinduliwa, mradi mmoja (1) umewekwa jiwe la msingi na miradi minne ( 4) imekaguliwa.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa