MWENGE WATEMBELEA BANDA LA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA KUONA SHUGHULI MBALIMBALI AMBAZO HALMASHAURI INATARAJIA KUZIFANYA KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.
Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imejipanga kikamilifu kuhakikisha zoezi la uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwaka 2024 linafanyika kikamilifu ili kupata viongozi bora katika vijiji vyote166 na vitongoji 886.
Juhudi Nkwama ni Afisa uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Masasi akisoma taarifa ya uchaguzi wa serikali za Mitaa kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa 2024 Ndg.Godfrey Eliakimu Mzava, amesema katika uchaguzi wa serikali za mitaa inategemea kupata wenyeviti wa vijiji, wenyeviti wa vitongoji na wajumbe wa Halmashauri za vijiji.
Amesema ili kufanikisha zoezi hilo muhimu kwa halmashauri na Taifa kwa ujumla, jukumu mojawapo la halmashauri ya Wilaya ya Masasi ni kuhakikisha inaweka mazingira rafiki yatakayowawezesha wananchi kupata taarifa sahihi zitakazo waelimisha na kuwahamasisha ili waweze kushiriki kikamilifu katika zoezi la uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Pia kuwashirikisha wananchi,Vyama vya siasa,Taasisi za umma na Taasisi za kijamii kwenye michakato mbalimbali inayohusu uchaguzi wa serikali za mitaa kwa kuzingatia kanuni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, katiba ya Jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, sheria ya serikali za mitaa (mamlaka ya Wilaya) sura ya 287, miongozo na maelekezo mbalimbali yatakayokuwa yanatolewa na mamlaka husika.
Aidha kiasi cha shilingi 50,000,000/= kimetengwa kwenye bajeti ya 2024/2025 kwa ajili ya zoezi hilo.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa