Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi na wadau kutoka Asasi za Kiraia wakiwa kwenye kikao cha kutaburisha mradi wa Mifumo ya Afya na Ustawi wa Jamii jana tatehe 07.06.2017 katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi
Uboreshaji wa mifumo ya kamati shirikishi za kudhibiti ukimwi kuanzia ngazi ya wilaya hadi kijiji kupitia mradi wa uimarishaji wa mifumo ya afya na ustawi wa jamii unaotekelezwa ofisi ya TAMISEMI kwa kushirikiana na shirika la John Slow Incorporation (JSI) linalosaidia masuala ya afya utasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma za afya na ustawi wa jamii kwa kutekeleza majuku yao ipasavyo.
Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mhe Juma Satmah kwenye kikao cha kutambulisha mradi huo wa kuimarisha mifumo ya afya na ustawi wa jamii kwa Halmashauri hiyo na kueleza kuwa mradi huo umekuja wakati mwafaka kwani kuna watoto wengi wanaoishi mazingira magumu na maambukizi ya virusi vya ukimwi ni makubwa kutokana na mwingiliano mkubwa uliopo.
Akitoa takwimu za maambuki ya Virusi vya ukimwi kwa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Satmah alisema kuwa kwa mwaka 2014 idadi ya watu waliopima Virusi vya ukimwi ni 29,554 wanawake 18400 na wanaume 11,154 na walikutwa na maambukizi ni 1140 wanawake 764 na wanaume 376. Kwa mwaka 2015 waliopima 33,152 waliokutwa na maambukizi ni 1189.
Pamoja na juhudi hizi bado maambukizi ni makubwa sana kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo mwingiliano mkubwa wa watu uliopo masasi hali inayopelekea maambukizi kuongezeka kwa kasi, hivyo mfumo huu utawezesha kamati kuanzia ngazi ya wilaya hadi kijiji kwa kiasi kikubwa kutoa elimu ya kutosha juu ya masuala ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi ili jamii iwe na afya njema kwa kufuata masharti ya umezaji dawa, kuboresha upatikanaji wa vifaa na kuwa na jamii yenye uelewa mpana kuhusu masuaa mazima ya ukimwi.
Mradi huu unatekelezwa na ofisi ya TAMISEMI kwa kushirikiana na shirika la JSI/CHSSP lengo ikiwa ni kuimarisha huduma kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na waishio na Virusi vya ukimwi ili kufikia lengo ikiwa kuboresha huduma hizo kwa asilimia tisini (90).
Mradi huu ni wa miaka mitano, ulianza kutekelezwa mwaka 2014 na jumla ya halmashauri 184 zitafaidika na mradi huu ikiwemo halmashauri ya wilaya ya masasi.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa