Wananchi wa kata za Mwena, Chikundi, Chigugu na Chikuwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wanatarajia kuondokana na tatizo la maji mara baada ya kukamilika kwa maradi wa maji wa MWENA –LILOYA unaotekelezwa sasa wenye thamani ya shilingi bilioni 4.4 na kutarajiwa kumalizika mwezi aprili 2018.
Akizungumza wakati wa ukauzi wa mradi huo Mhandisi wa Maji wa halmashauri hiyo ndugu francis Bwire alisema kuwa Mradi ukikamilika unatarajia kuwanufaisha jumla ya wananchi 66, 626 kutoka vijiji 18 wanaoishi katika Kata hizo ambao hawakuwa na huduma ya maji ya uhakika kwa muda mrefu.
Mbwire alieleza kuwa, katika mradi huo jumla ya vichotea maji 92 vinatarajiwa kujengwa katika vijiji 18 hivyo kufanya upatikanaji wa maji katika Halmashauri kuongezeka kutoka asilimia 51 hadi kufikia asilimia utakuwa umeongezeka kwa asilimia 23 na hivyo kufanya Halmashauri kuwa na asilimia 74.1
Akieleza hatua za utekelezaji, mhandisi bwire alisema kuwa mradi upo asilimia 25 ya utekelezaji ambapo shughuli za uchimbaji mtalo wa kulaza bomba, ulaziji wa bomba na ujenzi wa matanki ya kuhifadhia maji zinaendelea.
Pamoja na mradi huo wa MWENA – LILOYA, Mhandisi Bwire alisema Halmashauri pia inatekeleza mradi wa maji wa CHIPINGO -MKALIWATA katika Kata mbili wenye thamani ya shilingi bilioni 2.7 na unategemea kunufaisha watu 17420 katika vijiji 8 ndani ya Kata hizo mbili ambapo cha maji katika mradi huo ni mto Ruvuma.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa