Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mhe.Kanali Patrick Sawala amewataka Wananchi wote wenye sifa ambao bado hawajajiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura wa Serikali za Mitaa unatarajia kufanyika Nov 27,2024 kuendelea kujitokeza kujiandikisha kwenye vituo vilivyopo katika maeneo Yao ili wapate sifa ya kuchagua viongozi bora watakao waletea Maendeleo.
Mhe.Sawala amesema hayo Leo tarehe 16, 2024 katika muendelezo wa ziara yake ya kukagua na kuhamasisha uandikishaji katika Halmashauri za Mkoa wa Mtwara ambapo akiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ameweza kutembelea Kata ya Mpeta kwenye Kijiji Cha masuguru kitongoji Cha msikitini pamoja na Kijiji Cha mpeta ambapo pamoja na kuwasalimia Wananchi pia amepata fursa ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa Shughuli za uandikishaji wa orodha ya wapiga kura kutoka Kata ya Mpeta ambapo ameonyesha kufurahishwa na taarifa ya Kata nzima kuwa Wananchi wamehamasika kwa kiasi kikubwa kujiandikisha na wanajua umuhimu wa kujiandikisha na wapo tayari kuendelea kutoa hamasa kwa Wananchi ili waendelee kujitokeza kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura kwa siku zilizobakia ili waweze kufikia malengo.
"Nimekuja hapa ndugu zangu Pamoja na kuwasalimia lakini pia nimekuja kufuatilia ili kuona je Shughuli hii ya uandikishaji kwenye orodha ya wapiga kura Kwa ajili ya uchaguzi wa viongozi wetu wa Serikali za Mitaa, je unakwenda kwa utulivu, unakwenda kwa amani, je kuna changamoto zozote ili kama zipo tushauriane na kuona namna ya kuziondoa"... alisema Mkuu wa Mkoa
Amesema hata hivyo anayo furaha kubwa kuona zoezi hili la uandikishaji linakwenda kwa amani na utulivu,hakuna fujo Wala vurugu" hongereni sana wanampeta na Wana Masasi wote kwa ujumla kwa kufanya mchakato wa kujiandikisha kwa amani na utulivu"
Aidha mhe.Sawala ameongeza kuwa " inawezekana sisi tumejiandikisha Lakini wapo baadhi ya ndugu, jirani, marafiki n.k ambao wana sifa ya kupiga kura ikiwemo umri wa Miaka 18 na kuendelea, awe ni raia wa Tanzania, awe mkazi wa eneo husika na sifa Nyinginezo, hivyo nitoe rai kwenu wana Mpeta msifanye kosa tarehe 27 Nov,2024 wa kutokwenda kupiga kura, hamtakiwi kufanya majaribio, nendeni mkapige kura na kuwachagua viongozi watakao endana na hatua za mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, anataka nini kwa Wananchi wake, anaye jua matarajio na matamanio kwa Wananchi, kiongozi anaye jua kutafsiri nini matarajio ya mhe.Rais na hivyo kiongozi kiongozi atatoka miongoni mwenu.
"Niwaombe sana mkajiandikishe na mkisubiri kuchagua kiongozi Bora."
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Masasi ambaye pia ndiye Diwani wa Kata hiyo ya Mpeta Mhe.Ibrahimu Chiputula akizungumza kwaniaba ya Wananchi wa Kata hiyo amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kwa kuwatembelea na kuzungumza nao juu ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa hivyo wanahaidi katika siku chache zilizosakia wataendelea kuwahamasisha Wananchi kuendelea kujitokeza kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura ili ifikapo Nov 27,2024 watimize wajibu wao kikatiba kuwachagua viongozi Bora.
Hata hivyo, Zoezi la uandikishaji orodha ya wapiga kura limeanza rasmi Oktoba 11, 2024 na litahitimishwa tarehe 20,2024.
Ifahamike kuwa Kata ya Mpeta ambayo inaunda Vijiji 4 ambavyo ni Mpeta, Makanyama, Masuguru na Huwe
ni miongoni mwa kata 34 za Halmashauri ya Wilaya Masasi ambapo inapatikana katika Jimbo la Lulindi, tarafa ya Chiungutwa huku ikiwa na jumla ya idadi ya watu 5,871 Kati ya watu hao wanaune ni 2,779 na Wanawake 3,092. Aidha Kata ya Mpeta Ina jumla ya kaya 1,847 zenye wastani wa watu 3.2
@ Masasi DC
16/10/2024
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa