Moja ya choo ambacho kimetitia kutokana na kuta za shimo zake zilijengwa kwa kusimamisha tofali badala ya kulaza
Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri ya Wiaya ya Masasi Mkoani Mtwara bibi Changwa M Mkwazu ametoa siku tatu kwa kamati ya ujenzi wa mradi wa choo katika shule ya sekondari mbemba iliyopo Kata ya Chigugu katika halmashauri hiyo kubomoa kuta za shimo la mradi huo kutokana na kujengwa bila kufauata miongozo ya ujenzi wa vyoo unaotaka kulaza tofali wakati wa kujenga kuta za shimo la choo na sio kusimamisha kama walivyofanya wao.
Mkwazu ametoa agizo hilo leo wakati wa ziara endelevu ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo iliyopelekewa fedha na kuona kama inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa kitaalamu na kwa wakati ili iweze kutumika na kukuta kuta za shimo la choo katika shule hiyo likiwa limejengwa kwa kusimamisha matofali badala ya kulaza kama miongozo inavyoelekeza
Mkwazu alisema pamoja na kuwaeleza zaidi ya mara mbili kuhusu kubomoa kuta hizo wanakamati hawakutekeleza mpaka leo amekuta bado hawajabomoa na kuamua kuwapa siku tatu wawe wamebomoa kuta hizo na kuanza kujenga kwa kufuata miongozo ya kitaalamu kwa kutumia gharama zao na sio fedha ya halmashauri.
“Kama mtaendelea na ujenzi wa choo hiki bila kubomoa kuta za shimo la choo na kujenga kwa mujibu wa muongozo wa ujenzi wa vyoo bora, Halmashauri haitaleta fedha na mtatekeleza kwa gharama zenu na fedha zilizoletwa itabidi zirudishwe Halmashauri kwani kama serikali haiwezi kuleta fedha kwenye mradi usiozingatia viwango.
Aidha Mkwazu amewaambia kuwa halmashauri inatumia fedha nying kujenga vyoo kila mwaka lakini baada ya muda mfupi vinabomoka kwasababu vinajengwa kwa viwango vya chini lakini pia ni hatatari kwa wanafunzi kwani vyoo vingi vya namna hii vinatitia haraka sana kwani sio imara.
Aidha Mkurugenzi ametumia fursa hiyo kuwaasa viongozi wanaosimamia miradi yote ya umma inayotekelezwa kwa fedha za serikali na nguvu za wananchi kuzingatia miongzo ya ujenzi na wakikiwa hawaelewi ni vizuri kuomba ushauri kwa wataalamu wa sekta huska ili majengo yanayojengwa yaweze kudumu kwa muda mrafu.
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo mhe . Mpandula ameahidi kulifanyia kazi agizo hilo kwa haraka ili ujenzi uendelee na mradi uweze kukamilika na kutumika
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa