Wazazi na Walezi wenye watoto wanaosoma Shule za Msingi na Sekondari katika mikoa ya Lindi na Mtwara wametakiwa kuendelea kuchangia chakula mashuleni ili kuongeza ufaulu na kuimarisha hali ya Lishe kwa Watoto wao.
Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Ikulu (kazi maalumu) Mhe.George Huruma Mkuchika jana tarehe 08/08/2024 wakati akifunga maonyesho ya nane nane kanda ya kusini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ngongo -Lindi.
Amesema Pamoja Serikali kuwajengea Shule na kuboresha miundo mbinu mbalimbali katika Sekta hiyo ili kuona Watoto wanapata Elimu Bora pia kutoka kwa Wazazi wanataka kuona kila Mtoto anapata Lishe bora ili kumjengea kiafya hatua itakayosaidia kuwa na nguvu kazi ya kutosha kwaajili ya utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za miradi ya Maendeleo.
"Serikali imewajengea Shule na kuweka madawati, imeleta walimu, Wazazi tunaambiwa tuchangie chakula mashuleni kwa ajili ya watoto wetu ili waendapo Shule wapate uji,na chakula cha mchana kwasababu wao wanakaa mpaka jioni wakiwa Shule ".
Amesema takwimu zinaonyesha kwamba, "ndani ya mikoa yetu wapo Watoto ambao Wazazi wao hawakuchangia chakula, watoto wale wakati unapofika muda wa chakula wao hukaa pembeni na kuangalia wenzao wanaokula iwe uji au chakula cha mchana, ebu jifikirie kama ungekuwa ni wewe ungeweza? aliuliza...
Mkuchika ameendelea Kwa kusema kuwa Mtoto anayepata uji, chakula cha mchana uwezekano wa kufanya vizuri kwenye masomo yake ni mkubwa tofauti na yule Mtoto asiyepata chakula mashuleni na uwezekano ni mdogo wakufanya vizuri hivyo amesisitiza kaya zihakikishe zinajitosheleza kwa chakula na kuchangia mashuleni.
09 Aug 2024.
@.. Masasi DC..
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa