Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imeadhimisha siku ya Wanawake duniani katika Kata ya Ndanda huku Mambo matatu ya kumwezesha mwanamke ili kushiriki kwa vitendo kuelekea uchumi wa viwanda ifikapo 2025 ikiwemo kuwawezesha ķielimu, kuwapa mitaji na kuwashirikisha katika maamuzi yakisisitizwa.
Halmashauri ya wilaya ya Masasi kwa mwaka wa fedha 2017/2018 jumla ya shilingi milioni 79,445,000 zimekopeshwa kwa vikundi 31 vya wanawake ikiwa ni mitaji ya kuendeleza biashara zao na hivyo kuzalisha kwa tija ili kukuza uchumi wa kaya na Taifa kwa ujumla.
Kauli mbiu ya siku ya wanawake duniani mwaka 2018 unasema"KUELEKEA UCHUMI WA VIWANDA: TUIMARISHE USAWA WA KIJINSIA NA UWEZESHAJI WANAWAKE VIJIJINI"
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa