• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MILIONI 182 KUBORESHA MIUNDO MBINU YA SHULE ZA MSINGI-MASASI

Posted on: September 13th, 2018

Shule za Msingi Nakachindu na Chipango zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara  zilizokuwa na hali mbaya ya miundombinu ikiwemo madarasa na vyoo zitaondokana kabisa  na upungufu wa miundombinu hiyo  baada ya serikali ya Japani kupitia shirika lisilo la Kiserikali la Tanzania life improvement association (TALIA) kujenga madarasa 7 na matundu ya vyoo 12 katika shule hizo kwa gharama ya shilingi  milioni 182.

 Ujenzi wa Jengo la madarasa matatu katiaka shule ya msingi Chipango kwa msaada wa Serikali ya Japani  kwa kushirikiana na Shirika la TALIA

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa miradi hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Changwa Mkwazu alisema kuwa Halmshauri ina upungufu mkubwa wa miundombinu ya madarasa, vyoo na nyumba za walimu hivyo msaada huu ni mkubwa sana hasa kwenye shule hizi mbili ambazo ziliuwa na  hali mbaya sana.

Mkwazu alikiri kuwa “Shule ya Nakachindu ilikuwa na madarasa mawili tu Halmashauri mwaka jana ilijenga darasa moja yakawa matatu lakini bado haikukidhi mahitaji ilikuwa ni wakati mugumu kwa walimu na wanafunzi maana iliwabidi wanafunzi wa madarasa tofauti kusoma katika darasa moja”

Ujenzi wa madarasa haya utamaliza kabisa upungufu wa vyumba vya madarasa na vyoo katika shule hizo kwani kila darasa litakuwa na chumba chake tofauti na hapo awali ambapo wanafunzi wa madarasa tofauti walitumia chumba kimoja kusomea.

Aidha Mkwazu ameishukuru Serikali ya Japani na shirika la TALIA kwa kuweza  kuona uhitaji mkubwa wa miundombinu ya shule na kuamua kusaidia  ujenzi wa madarasa 7 na vyoo matundu 12 ya kisasa kabisa katika shule za Nakachindu na Chipango kwani serikali pekee haiwezi kumaliza tatizo hilo

Kwa upande wake msimamizi wa mradi kutoka Ubalozi wa Japani nchini Tanzania  Mai Yamazaki alisema kuwa umekuwa ukichangia fedha katika miradi mbalimbali ya Maendeleo katika sekta ya Afya, elimu na maji tangu mwaka 1991 lengo ikiwa ni kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha huduma za jamii kwa wananchi.

Mwakilishi wa ubalozi wa Japani nchini Tanzania (wa kwanza kulia) akitoa maelezo wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule ya  msingi Nakachindu

Mai alifafanua kuwa “ miundombinu ya madarasa na vyoo inayojengwa katika shule hizi ni ya kisasa kabisa ambapo itakuwa na madilisha ya vioo, umeme na yataezekwa kwa mabati ya kisasa, lengo ni kuyafanya mazingira ya shule kuwa mazuri lakini pia wanafunzi kuwa na mazingira bora ya kusomea”

Nae Kaimu Afisa Elimu Msingi ndugu Eugine Ngaeje alieleza kuwa   Halmashauri iliainisha shule zenye matatizo kwa shirika la TALIA na kufanya ukaguzi katika shule hizo,  ndipo shule za nakachindu na chipango zikakaonekana kuwa na shida kubwa zaidi “ tunawashukuru sana kwa msaada wao maana umeondoa kabisa tatizo la upungufu wa vyumba vya madarasa na vyoo, tunategemea walimu na wananfunzi watakuwa na mazingira mazuri ya kujifunza na kujifunzia.

Aidha Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nakachindu Fortunatus Nichelewa ameishukuru serikali ya Japani na shirika la TALIA kwa kuweza kukubali kutoa fedha za ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule yake kwani shule ilikuwa na madarasa matatu tu lakini baada ya kukamilika hakutakuwa na upungufu tena.

Mwakilishi wa ubalozi wa Japani nchini Tanzania (wa katikakti) akitoa maelezo  Mkurugenzi Mtendaji wa H/W , wawakilishi wa shirika la TALIA  na watumishi wengine wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa madarasa na vyoo katika shule ya  msingi Chipango

Nichelewa alieleza kuwa “hali ilikuwa mbaya sana wanafunzi wa madarasa yote kutumia vyumba vitatu vya madarasa, chumba kimoja wanatumia wanafunzi wa madarasa matatu hali ambayo ilipelekea usikivu kuwa mdogo sana”

Halmashauri ya wilaya ya masasi ina upungufu wa madarasa 802 , matundu ya vyoo 582 na nyumba za walimu 1206 kwa upande wa shule za msingi

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • MSIGWA: MAAFISA HABARI NI SAUTI YA SERIKALI, TANGAZENI MAFANIKIO YA SERIKALI KWENYE MAENEO YENU.

    May 25, 2025
  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI MNAKUWA WABUNIFU NA WAZALENDO ILI WANANCHI WAPATE HABARI SAHIHI NA KWA WAKATI.

    May 23, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MASASI DC KWA KISHINDO:WATEMBELEA MIRADI MITANO YENYE THAMANI YA TSH.MILIONI 678,844,040.00

    May 19, 2025
  • WATENDAJI WA SERIKALI TEKELEZENI WAJIBU WENU WA KIKAZI,MSIJIHUSISHE NA MAMBO YA SIASA: BARAZA LA MADIWANI

    May 15, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa