Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara amewapongeza watumishi 15 waliochaguliwa kuwa wafanyakazi bora kwa mwaka huu 2018 kwa kuwapa zawadi ikiwa ni njia ya kutambua utendaji kazi wao.
Zawadi hizo zilitolewa kwa watumishi hao siku ya wafanyakazi duniani maarufu kama Mei Mosi iliyoadhimishwa kimkoa wilayani Newala katika viwanja vya sabasaba.
Watumishi bora hao wametoka katika idara mbalimbali baada ya kuona utendaji wao kuwa bora zaidi, hivyo Halmashauri ikaamua kuwapongeza katika sherehe ya wafanyakazi duniani maarufu kama mei mosi kwa kuwapa zawadi ikiwa ni njia ya kutambua mchango wao katika utumishi wao
Kauli mbiu ya maadhimisho ya mei mosi mwaka huu 2018 "Kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii kulenge kuboresha mafao ya wafanyakazi"
Mwaka 1884 shirikisho la vyama vya wafanyakazi wa Marekani (American Federation of Labour) liliitisha mkutano mkuu. Azimio likapitishwa kuwa kufikia Mei Mosi 1886 kikomo cha saa nane kwa siku na ndio maana siku hii husherekewa duniani kote ambapo watumishi hutumia siku hii kusherekea
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa