Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa Mtwara Mhe.Agnes Hokororo Leo tarehe 25/09/2024 ameongoza zoezi la ugawaji taulo za kike kwa wanafunzi wa Shule za Msingi na Sekondari zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi huku akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi.Beatrice Mwinuka kwa kutenga fedha za ndani kwa ajili ya ununuzi wa taulo za kike.
Zoezi hilo ambalo ni endelevu katika Shule zote zilizopo Halmashauri ya Wilaya Masasi, pamoja na mambo mengine limeanzia katika Kata ya Mbuyuni na wanufaika wa msaada huo ni wanafunzi shule ya Msingi mbuyuni, Mitonji pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mbuyuni.
Akizungumza kabla ya ugawaji wa taulo hizo kwa wanafunzi hao wakike ambao wame wawakilisha wanafunzi wa shule zingine mhe.Hokororo ameanza kwa kumpongeza na kumshukuru Mkurugenzi Mtendaji pamoja na timu yake nzima ya Uongozi kwa kuchukua hatua ya kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa taulo za kike katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
Amesema Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa kuzingatia maelekezo ya Serikali kwamba kila Halmashauri lazima itenge fedha hivyo na Kwa kuona umuhimu imeweza kuweka bajeti ya shilingi Milioni 20 na kuanza kununua taulo za kike kwa ajili ya kuwastili Watoto wakike ambao wanakumbana na changamoto mbalimbali na hasa wakiwa katika mazingira ya shuleni.
" Hivyo rai yangu kwa Halmashauri iendelee kutenga fedha za ndani kupita mfuko wa elimu kwasababu kwa kufanya hivi zitaendelea kuwasaidia Watoto wetu wa shule za Msingi na Sekondari ".
Aidha mhe.Hokororo akatumia fursa hiyo pia kuzungumza na Wazazi/walezi ambao wamejitokeza katika zoezi hilo la ugawaji wa taulo za kike kwa wanafunzi, ambapo amewakumbusha Wazazi watambue kuwa watoto wana haki za msingi na ipo Sheria inayowalinda ambayo imetungwa na bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikielekeza kupitia haki ya Kwanza ya kuishi kwa kuwapatia chakula, malazi na mavazi.
" haki ya pili ni kuwalinda kwa kuhakikisha mambo yao yote na ustawi wa watoto unakuwa chini yenu Wazazi na kuwahakikishia usalama kwa kuwalinda na kuwapatia mahitaji yao ya msingi hususani taulo za kike ambazo ni moja ya mahitaji muhimu ambayo Mtoto anatakiwa kuwa nayo hivyo ni wajibu wenu kuhakikisha Watoto wanatimiziwa mahitaji hayo."
Bi.Ashura Mrope ni mzazi Pamoja naye Vaileth Sijaona ambaye ni mwanafunzi pamoja na kushukuru kupatiwa Elimu ya afya na malezi kwa Watoto pia wameshukuru kwa msaada huo wa taulo za kike walizopatiwa wanafunzi hao kuwa utawasaidia kujistiri katika siku zao na hasa siku za masomo tofauti na hali ya sasa huwa mara nyingi wanabaki nyumbani na kufanya kukosa vipindi.
25/09/2024
@.. Masasi DC
Kazi iendeleeee!
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa