UTOAJI WA CHANJO MPYA YA KUZUIA SARATANI YA MLANGO WA KIZAZI
Utoaji wa chanjo mpya ya kuzuia saratani ya Mlango wa kizazi kwa wasichana wenye miaka 14 nchini ilizinduliwa tarehe 10 Aprili .2018 ambapo kwa wilaya ya Masasi utoaji wa chanjo hiyo ilizinduliwa tarehe 23 aprili 2018 Lengo la utoaji wa chanjo hii ni kupunguza vifo vya wanawake vitokanavyo na saratani ya Mlango wa kizazi.
Utoaji wa chanjo hii kwa wasichana wenye umri wa miaka 14 waliodhuleni na wasiosoma ni kwasababu wanakuwa bado hawajaanza kufanya ngono ambayo ndio sababu kubwa ya kuenea kwa ugonjwa huu, hivyo kama wakipewa chanjo hawatakuwa na hatari ya kuambukizwa saratani hii na hivyo kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi kwa wanawake.
Huduma hii ni bure na inatolewa katika vituo vya kutolea Huduma za kutolea Huduma za afya, shule za msingi na sekondari na maeneo yanayotolewa huduma ya mkoba katika maeneo vijiji, Kata na ngazi ya wilaya.
Ifahamike kuwa kila mwaka wanawake 466,000 duniani hupata maambukizi ya ugonjwa wa saratani ya Mlango wa kizazi huku Kati ya hao wanawake 50,000 ni kutoka Tanzania. Hivyo kwa Wazazi na walezi ni jambo jema kuwaruhusu watoto wa kike wenye umri wa miaka 14 kupata chanjo hii kwa ni salama.
Chanjo hii inazuia tu maambukizi ya saratani ya Mlango wa kizazi na sio magonjwa mengine kama UKIMWI na magonjwa ya zinaa hivyo ni vizuri watu waache Ngongo zembe kwani unaweza kuzuia saratani ya Mlango wa kizazi lakini ukapata magonjwa mengine kama UKIMWI unayoambukizwa kwa njia ya ngono.
Kwa mwaka huu Wilaya ya Masasi inatarajia kutoa chanjo kwa wasichana wenye umri miaka 14 waliozaliwa Kati ya January hadi disemba 2004 wapatao 3, 708 ambapo hadi kufikia tarehe 27 Aprili, 2018 jumla ya wasichana 1234 sawa na asilimia 33.3
Chanjo hii inatolewa kwa dozi mbili ambapo dozi ya kwanza atapatiwa wakati wowote anapotimiza miaka 14 na dozi ya pili anapata baada ya miezi sita tangu alipopatiwa dozi ya kwanza.
"Jamii iliyochanjwa ni jamii yenye afya" afya yangu, mtaji waji"
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa