Matukio katika picha inawaonyesha Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara wakikabidhi zawadi mbalimbali kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mara baada ya kuhitimisha kwa ziara yao ya kimafunzo waliyoifanya mapema februari 12,2025 katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
Miongoni mwa Zawadi hizo ni pamoja na Korosho, Ufuta, Mbaazi, Miche 200 ya mikorosho, pamoja na Vinywaji vinavyotokana na mabibo (Mabibo Wines).
Hata hivyo ikumbukwe kuwa Wilaya ya Kondoa imefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa lengo la kujifunza namna bora ya uanzishwaji na utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi ghalani ambapo kwa Halmashauri ya Wilaya Masasi ni moja ya Halmashauri inayofanya vizuri sana katika suala la uuzaji wa mazao ya Wakulima kupitia mfumo huo maalumu wa Stakabadhi ghalani jambo ambalo linawapelekea Wakulima wenyewe kunufaika na Mazao yao huku Halmashauri nayo ikiongeza Mapato yake kwa asilimia kubwa.
13/02/2025
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa