Mkuu wa wilaya ya masassi Suleimani Mzee ametoa pongezi kwa wafanyakazi bora ambao wamekabidhiwa zawadi leo hii katika Halmashauri ya wilaya ya masasi kutoka katika idara na vitengo mbalimbali na kuwakumbusha kuendelea kuchapa kazi kwa bidii bila kubweteka ili juhudi,na , ufanisi wao wa kazi uendelee kuleta tija katika maeneo yao ya kazi. aliendelea pia kwa kuwapongeza
wanakikundi ambao wamepatiwa asilimia kumi ya mkopo wa halmashaur kutumia vizuri mikopo hiyo ilil malengo waliojiwekea waweze kufanikiwa na kuboresha maisha yao na familia zao na kuwataka maafsa mipago ,kutembelea vikundi hivyo.ili kubaini changamoto zao na kuzitafutia ufumbuzi
Ameeleza hayo leo hii katika sherehe ya siku malum ya halmashauri ya wilaya ya masasi ambayo imeandaliwa na mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa lengo la kujumuika kwa pamoja na watumishi wote kutoa mikopo ya asilimia kumi kwa wanawake ,vijana,na watu wenye ulemavu kama agizo la serikali linavyozitaka halmashauri zote nchini kutoka katika mapato ya ndani pamoja na kutoa zawadi kwa watumishi bora kutoka idara na vitengo mbalimbali ikiwa ni njia mojawapo ya kuinua ari na ufanisi kazini miongoni mwa watumishi.
Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya masasi ndg Ibrahimu issa chiputula ametolea ufafanuzi lengo la kuandaa sherehe hiyo na kuwaomba walimu wa ajira mpya wapatao 68 kuwa na busara kwa maeneo waliyopangiwa kazi, na kutoa msisitizo kwa vikundi walivyopatiwa mikopo kurejesha kwa wakati ili na watu wengine waweze kupata mikopo hiyo .
Sambamba na hayo wanavikundi walopatiwa mikopo hiyo pamoja na maafisa watendaji kata walokabidhiwa pikipik walitoa shukran kwa halmashauri na kueleza mipango mikakati waloiwekea katika kurejesha mikopo na kuleta maendeleo katuka kata zao na halmashauri
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashaur ya Wilaya ya Masasi Bwana Lyoba Magabe alitolea ufafanuzI lengo la kuandaa siku hii ambayo ilikuwa ni siku maalumu ya Halmashaur ya wilaya ya masasi ni kukabidhi Mikopo kwa vikundi 52 ,kukabidhi zawadi kwa wafanya kazi Bora 22,kukabidhi Godoro kwa walimu 68 walioajiliwa ajira mpya katika Halmashaur hiyo,kukabidhi zawadi kwa wanafunzi na walimu wao wa shule ya Sekondari Mkalapa waliofanya vizuri katika mchezo wa Kikapu maarufu kama volleyball na kuitangaza Masasi na Mkoa wa Mtwara kupitia michezo ,kukabidhii pikpiki 18 Kwa watendaji wa kata.
Kutokana na hayo kaimu mkurugenzi alieleza kuwa Halmashauri yetu imeweza kuibuka na kuwa kinara katika ukusanyaji mapato kati ya halmashauri zote nchini ushindi uliopatikana ni kutokana na usimamizi mzuri wa kudhibiti mapato na kuongeza kuwa watendaji kata na vijiji pia ni chanzo kikubwa katika mafanikio haya na kuishukuru na kuipongeza timu ya mapato ya Halmashauri kwa utendaji kazi wake na kuwa sehemu ya mafanikio haya.
Mwalimu huyu akipokea zawadi ya Godoro kwa niaba ya wenzake 68 ambao ni ajira mpya kwa mwaka huu 2021 kwa shule za msingi walimu 40 na sekondari walimu 28 ili waanzie maisha lakini kama sehemu ya motisha kwa walimu wapya mpango ambao umekuwa ukiendelea kufanywa na Halmashauri.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Mkalapa ambao pia ni wachezaji wa timu ya kikapu inayowakilisha Mkoa wa mtwara katika mashindano mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na Meza kuu baada ya kutunikiwa vyeti maalumu na zawadi mbalimbali ikiwemo vifaa vya shule .
Wazazi wa wanafunzi wa shule ya mkalapa ambao ni wachezaji wa Mpira wa nyavu walitoa shukrani zao kwa HalmashaurI kwa zawadi walizotunukiwa siku hii na kuiomba serikal kuwawezesha zaidi ya hapa walipo ili waweze kufika mbali zaidi ya hapa.
Watendaji wa kata 18 wakikabiziwa pikipiki zao leo na mgeni rasmi Mh. selemani Mzee kwa niaba ya mkuu wa Mkoa wa Mtwara tayari kwenda kuzitumia ili ziweze kuwarahisishia utendaji kazi wao zilizonunuliwa kwa mapato ya ndani.
Neema josephu ambaye ni afisa maendeleo ya jamii wa halmashaur ya wilaya ya masasi ameeleza Kama idara ya maendeleo kupitia halmashauri hiyo kuwa wametoa mikopo ya asilimia kumi kwa wanawake,vijana,na watu wenye ulemavu kwa kutekeleza agizo la serikali kwa mwaka 2020/202, Kama halmashauri wamepanga kutoa Milion 207 kutoka kwenye mapato ya ndani
Na mikopo hii ilotolewa 23 January, wamekabidhi pesa taslim sh milioni 191 kwa vikundi 52 kwa lengo la kuwainua wanavikundi mbalimbali Kwa upande wa changamoto za mikopo ilopita neema alieleza kuwa walitoa mikopo yenye thaman ya sh BilionI moja na zaidi lakini ulipaji wa mikopo hiyo ni mdogo walikusanya Milion 800 na pesa zilizobaki ni Milion 200 katika vikundi hivyo
Kutoka na changamoto hiyo Kama kitengo Cha maendeleo wanaendelea kutoa elimu kwa wanakikundi kujikita katik shughuli za kimaendeleo ambazo zinaweza kujiingizia kipato ili waweze kulipa maden hayo kwa wakati.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa