Jumla ya makosa 21 ya dawa za kulevya aina ya bhangi yenye uzito wa kilogramu 171 na gramu 262 yalikamatwa, aidha kesi 14 zimefanikiwa mahakamani, kesi 04 zinaendelea mahakamani na kesi 03 zipo chini ya upelelezi .
Jumla ya watuhumiwa waliokamatwa kuhusiana na makosa hayo ni 25 ambapo kati ya hao wanawake ni 02 na Wanaume 23.
Kwa kipindi cha mwezi January hadi April 2023 na kipindi kama hicho mwaka 2024 Mapambano hayo dhidi ya biashara haramu na matumizi ya dawa za kulevya yamekuwa yakifanyika kwa kupitia doria, misako na utoaji elimu kwa jamii.
Hayo yamebainishwa katika taarifa ya mapambano dhidi ya madawa ya kulevya iliyowasilishwa kwa mkimbiza mwenge wa uhuru kitaifa Godfrey Eliakimu Mzava, ambapo taarifa inaeleza kuwa katika eneo hilo aina ya dawa za kulevya wanazopambana nazo ni bhangi,Cocaine,Heroine na Mirungi ingawa sasa Cocaine,Heroine na mirungi ni kwa kiasi kidogo sana.
Aidha zimeelezwa zipo athari mbalimbali za madawa ya kulevya kama vile kushuka kwa uzalishaji mali kwa taifa na ufanisi, kuenea kwa magonjwa kama afya ya akili,uraibu, moyo,HIV, homa ya ini, kuongezeka kwa makosa ya jinai, kupoteza kumbukumbu, utegemezi, kupelekea vifo, n.k
Pamoja na hayo elimu kuhusu dawa za kulevya imeendelea kutolewa kupitia vipindi mbalimbali vya polisi jamii, radio,Wasanii,Wazee wa kimila(Mamwenye) na viongozi wa kidini yaani (SPRITIUL PATROL) kwa kushirikina na polisi kata kuelimisha madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya na athari zake dhidi ya afya za watumiaji.
Hata hivyo kwa kuhitimisha taarifa hiyo kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2024 akatembelea banda na kujionea shughuli mbali mbalimbali zinazofanywa na mapambano ya madawa ya kulevya.
Kazi iendelee!
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa