Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Desemba 13, 2024 imekabidhi Magari manne pamoja na Pikipiki Tisa kwa Halmashauri zilizopo mkoani Mtwara kwa ajili ya kufuatilia huduma za Chanjo mkoani humo.
Akikabidhi Magari hayo kwa Wakuu wa Wilaya ambazo Halmashauri zao zimepata Magari hayo, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Kenan Sawala, ameipongeza Serikali kwa kutoa Msaada wa Magari na Pikipiki hizo.
Kanali Sawala ameongeza kuwa, upatikanaji wa Vyombo hivyo vitatumika katika kuwafikia Watoto zaidi ya Elfu 70, Wanawake wajawazito zaidi ya Elfu 73 na Wasichana zaidi ya Elfu 20 ambao watapata Chanjo itakayozuia Saratani ya Kizazi kwa mwaka.
Hata hivyo RC Sawala amezitaja Halmashauri zinazopata Magari hayo kuwa ni Nne ambazo ni Mtwara DC, Nanyamba TC, Masasi DC na Newala DC huku Halmashauri zote 9 zikipata Pikipiki moja moja ambapo kwa mgao huo tayari Mkoa una Jumla ya Magari Manane ya usimamizi wa huduma za chanzo.
Kwa upande wake Kaimu Katibu tawala mkoa wa Mtwara Bi Nanjiva Nzunda amesema Halmashauri pekee iliyobaki kupata Gari ni Halmashauri ya Wilaya ya Newala ambayo pia watapata mgao huo.
Nae Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mtwara mikindani Mhe. Shadida Ndile, ameishukuru Serikali kwa kutoa Magari hayo huku akiahidi kushirikiana na Watendaji wengine katika kuyatunza Magari hayo.
13/12/2024
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa