Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Masasi limeidhinisha bajeti ya Tshs.31,147,559341.00 kwa mwaka wa fedha 2017/2018 kutoa vyanzo vyake mbalimbali za mapato ambapo 4,173,696,000.00 kutoka mapato ya ndani na 26,973,863,341.00 ruzuku kutoka serikali kuu.
Akiwasilisha mpango wa bajeti hiyo kwa mwaka 2017/2018 Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo ndugu Jeremiah Lubeleje aliwaeleza wajumbe kuwa mpango wa bajeti umezingatia sheria ya bajeti ya mwaka 2015 na imejikita zaidi kuteleza mambo mbalimbali ikiwemo umaliziaji wa miradi viporo jambo ambalo limekuwa changamoto kwa halmashauri hiyo.
Akichangia hoja ya miradi viporo katika halmashauri hiyo makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo Diwani wa Kata ya Mpanyani mhe, leodgar Chilala alisema kuwa utengaji wa bajeti ndogo kwenye miradi ni sababu kubwa ya miradi mingi kutokukamilika katika mwaka husika.
Pamoja na utengaji mdogo wa bajeti lakini pia maagizo mengi ya kitaifa ikiwemo ujenzi wa maabara na utengenezaji wa madawati umechangia kwa kiasi kikubwa miradi mingi iliyokuwa kwenye bajeti kushindwa kutekelezeka alisema Chilala
Aidha Lubeleje aliwaeleza wajumbe kuwa suala la miradi viporo limekuwa sugu kutokana na mwamko mdogo wa wananchi kuchangia nguvu katika kutekeleza miradi wakati miongozo inaelekeza wananchi kuchangia asilimia 20 kwenye utekelezaji wa miradi katika maeneo yao
Lubeleje alisema kuwa “wananchi hawachangii nguvu zao hali inayopelekea fedha inayopelekwa kutekeleza mradi inatumika kufanya shughuli zote hata zile ambazo mwananchi alitakiwa kufanya kama kukusanya mchanga, mawe na kuchota maji wakati wa ujenzi ili kupunguza gharama hatimaye mradi haukamili
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa