Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya Masasi Bi.Beatrice Mwinuka pamoja na Afisa Uchaguzi wa Halmashauri hiyo Bw.Juhudi Nkwama leo tarehe 17/10/2024 wamekutana kwa pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa kutoka ndani ya Halmashauri hiyo huku wakiwajulisha mabadiliko madogo ya ratiba ya matukio ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024.
Awali akizungumza katika kikao hicho ambacho kimefanyikia katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri hiyo uliopo Masasi mjini, Msimamizi wa Uchaguzi Halmashauri ya Wilaya Masasi Bi.Beatrice Mwinuka amesema wamepokea maelekezo Kutoka Ofisi ya katibu Tawala Mkoa wa Mtwara ikiwaelekeza mabadiliko machache ambayo yametolewa na Ofisi ya Rais Tamisemi kuhusu ratiba ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatarajia kufanyika Nov 27,2024.
Amesema " mabadiliko hayo ni pamoja na Ukomo wa madaraka (viongozi) wenyeviti wa vijiji, wenyeviti wa vitongoji na Wajumbe wa Halmashauri za Vijiji ambao badala ya kuwa tarehe 25 Oktoba 2024 sasa Madaraka Yao ya Ukomo itakuwa ni tarehe 19/10/2024"
" Jambo lingine ni tarehe ya kuanza kuchukua fomu za uteuzi ili wapate wagombea watakaosimama kwenye nafasi mbalimbali ambazo zitafanyiwa uchaguzi katika Siku ya Uchaguzi, na badala yake Sasa itakuwa ni tarehe 26 Oktoba 2024 - 01 Nov 2024."..alisema Mwinuka
Naye Afisa Uchaguzi wa Halmashauri hiyo Bw. Juhudi Nkwama pamoja na kuwapa ufafanuzi kuhusu suala la uapishaji mawakala kwamba zoezi hilo ni endelevu katika kipindi hiki cha uandikishaji ambapo mheshimiwa hakimu au wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata, vijiji au Mitaa wanaweza kukasimu ili kurahisisha mchakato huo, pia wamewasisitiza Viongozi hao kuzingatia sheria na taratibu katika kuendesha michakato mbalimbali inayohusu uchaguzi, kwaiyo " kikao kilikuwa kizuri na wamehaidi kutoa ushirikiano huo".
Hata hivyo Bw. Nkwama akatumia fursa hiyo pia kuendelea kuwaomba Wananchi wote wa Halmashauri ya Wilaya Masasi ambao bado hawajajiandikisha watumie muda uliobaki kuhakikisha wanajiandikisha ili wapate sifa za kuwachagua viongozi wanaowataka siku ya Uchaguzi, Lakini pia hata wale ambao tayari wamejiandikisha watumie muda huu kuwahamasisha wenzao kwasababu wanajuana.
17/10/2024
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa