Maafisa ugani wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wametakiwa kuwa na mashamba darasa katika maeneo yao ili kuwaelimisha na kuwashauri wakulima kwa vitendo juu ya teknologia mbalimbali za kilimo ambazo zinalenga kuboresha kilimo na kuongeza uzalishaji.
Hayo yamesemwa leo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Changwa M. Mkwazu akifunga mafunzo kwa maafisa ugani wa Halmashauri hiyo juu ya matumizi ya teknolojia mblimbali za kilimo, yaliyoendeshwa na wataalamu wa wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi lengo ikiwa ni kuwafundisha matumizi ya teknlogia hizo za kilimo ikiwemo uzalishaji wa mbegu zinazokabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Mkwazu alisema kuwa wakulima wanahitaji sana ushauri wa maafisa ugani katika uzalishaji wa mazao mbalimbali ili waweze kuzalisha kwa wingi ikiwemo ushauri juu ya matumizi ya mbegu bora, matumizi ya madawa ya kuua wadudu wanaoshambulia mazao maana hayo ni mambo muhimu mkulima kuzingatia wakati wa kilimo ili aweze kuzalisha kwa tija.
“Kama afisa ugani hautatumia taaluma kubadilisha wananchi kupitia kilimo hata uwe na elimu kubwa haita kuwa na faida kwa mwananchi, ni vizuri tubadilike kuweni na mashamba darasa ambayo wakulima watajifunza kwa vitendo” alisema mkwazu.
Japo kuwa wakulima wanatumia nguvu nyingi kulima lakini uzalishaji umekuwa mdogo sana kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo matumizi ya teknolojia duni pamoja na mabadiliko ya tabia ya nchi yanayosababisha ukame, magonjwa mabalimbalina wakati mwingine mvua kuzidi kiwango.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa