Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Bibi Changwa Mkwazu amewata maafisa Ugani wa Halmashuri hiyo kutumia utaalamu wao ipasavyo katika kuendeleza sekta kilimo hususani zao la korosho na ufuta ambayo ndiyo mazao yanayotegemewa zaidi kama chanzo cha mapato kwa wakulima na halmashauri.
Mkwazu ametoa kauli hiyo leo kwenye kikao cha maelekezo kwa maafisa ugani hao na kueleza kuwa silimia 90 ya mapato ya Halmashauri yanatokana na kilimo huku korosho ikichangia kwa asilimia 70 , hivyo “ tambueni kuwa hii ni sekta muhimu sana kwa Halmashauri kwani fedha nyingi za utekelezaji wa miradi ya maendeleo zinatokana na mapato yatokanayo na sekta ya kilimo “
Mkwazu amewasisitiza wataalamu hao wa kilimo ngazi ya kata kuwahamasisha na kuwashauri wakulima wote wa zao la korosho kuanzisha mashamba mapya, kupanda miche mipya, kubebesha, kupanda kwa msitari na nafasi inayotakiwa, kupalilia pamoja na kufanya upuliziaji kwa wakati
Maafisa ugani wakifuatilia maelekezo leo tarehe 18.08.2020 kwenye kikao cha kukumbushwa majukumu yao
“Tembeleeni wakulima, wapeni ushauri na hamasisheni walime kilimo cha kisasa na chenye tija ili kuongeza uzalishaji ndani ya halmashauri” amesistiza Mkwazu
Aidha Afisa kilimo, umwagiliaji na ushirikiano wa Halmashauri hiyo ndugu Winfrid Tamba ameeleza kuwa moja ya mkakati wa idara ni kuongeza uzalishaji wa zao la korosho kwa mti mmoja kutoka kilo 10 kwa sasa mpaka kilo 30 kwa mti mmoja, pia kuanzisha mashamba mapya ya korosho ili kuongeza idadi ya mikorosho kutoka miti milioni 4.08 hadi milioni 4.6 ifikapo 2023
Tamba amesema kuwa, kwa sasa Halmashauri inazalisha jumla ya tani 26,191 za korosho msimu wa 2019/2020 ukilinganisha na tani 24,000 zilizotegemewa kukusanywa.
Kwa upande wake Afisa Mazingira wa Halmashauri hiyo , bibi Kulwa Maiga amewaomba maafisa ugani kuzingatia kilimo endelevu ambacho ni rafiki kwa mazingira mfano kilimo msitu ambacho kinahifadhi mazingira ukizingatia kwa sasa kiwango cha matumizi ya madawa ya kilimo kimeongezeka sana
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa