Siku ya Utumishi wa Umma Barani Afrika ni siku maalum ya Watumishi wa Umma na taasisi zote za umma ambayo huadhimishwa na nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) ifikapo juni 23 kila mwaka.
Maadhimisho haya yamelenga kutambua mchango wa Watumishi wa umma katika Maendeleo ya Bara laAfrika.
Ikumbukwe kuwa chimbuko la sherehe za Maadhimisho hayo ni matokeo ya uamuzi wa mkutano wa Mawaziri wenye dhamana ya Utumishi wa Umma uliofanyika Tangiers huko Morocco mnamo mwaka 1994, ambapo uamuzi huo ulizitaka nchi za Afrika kusherehekea sherehe hizo huku wakiwa na kauli mbiu moja katika bara zima la Afrika.
Hata hivyo katika kuendelea kulifanikisha hilo, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi inashiriki kikamilifu katika Maadhimisho hayo ya wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika kuanzia tarehe 16 juni 2025 hadi tarehe 23 juni 2025 kwa kutoa huduma mbalimbali kwa Watumishi pamoja na wadau zikiweno masuala ya Utumishi na Utawala, Msaada wa kisheria, Elimu ya Haki za binadamu na Elimu ya uraia na utawala bora.
Fursa nyingine inayotolewa ni utoaji wa Elimu ya mfumo wa NeST, Tausi, Ess, Psssf Portal , Planrep n.k
Halmashauri ya Wilaya Masasi inaendelea kuwakaribisha Watumishi wote wa umma pamoja na wadau kutumia fursa hiyo kufika katika Ofisi za zamani za Halmashauri hiyo zilizopo Masasi mjini ili kupata huduma mbalimbali.
Wiki ya Maadhimisho ya Utumishi wa Umma inaongozwa na kauli mbiu isemayo "Himiza Matumizi ya Mifumo ya Kidijitali Kuongeza upatikanaji wa Taarifa na Kuchagiza uwajibikaji "
17/06/2025
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa