Ili kuwa na jamii yenye watu wenye uwezo mzuri wa kufikiri na afya bora, Suala la lishe bora na kupata huduma za afya kwa mama mjamzito ni muhimu kuanzia kipindi cha ujauzito na baada ya ujauzito kwa kuwa ndio msingi wa afya bora kwa mtoto kimwili na kiakili.
Hayo yalizungumzwa na meneja wa mradi wa Agha khan Foundation ndugu Biko Evaristy wakati wa hafla fupi ya kukabidhi mradi wa kuboresha huduma za afya uliotekelezwa katika kata sita ambapo pamoja na kutoa elimu ya lishe na unyonyeshaji watoto pia waliweza kujenga miundombinu ya kuvuna maji ya mvua katika vituo vya kutolea huduma lengo ikiwa ni kuhakikisha utoaji wa huduma za afya unakuwa wa kuridhisha.
Biko alieleza kuwa kati ya vitu vinavyoathiri watu wengi ni lishe duni inayopelekea utapiamlo, kwani inakadiliwa zaidi ya watoto milioni 180 duniani wenye umri chini ya miaka mitano wamedumaa kiakili na kimwili kwa kusosa lishe bora hali inayopelekea watoto kuwa na uwezo mdogo wa kufikiri na kujifunza kuwa mdogo.
Kiafya, Uzingatiaji wa Lishe bora unafanyika ndani ya siku 1000 yani tangu mama anapata ujauzito hadi mtoto anapofikisha umri wa miaka miwili, kwani ndio namna pekee ya kuhakikisha mtoto anakua vizuri kwa kunyonyeshwa vizuri na kupata lishe bora ili kumwepuka mama na mtoto kupata matatizo ya kiafya na kiakili ikiwemo utapiamlo, udumavu kwashakoo, ugonjwa unaotokana na kupunguza au kuzidisha mahitaji muhimu katika mwili
Kwa mujibu wa Afisa lishe wa Halmashauri ya wilaya ya masasi ndugu Victoria Ngatunga ilifafanua kuwa, Kuna aina mbalimbali za utapiamlo ambazo mtoto anaweza kuzipata ikiwemo utapiamlo wa kukonda, utapiamlo wa ufupi na hali hiyo huwa hivyo mpaka kwenye maendeleo ya ubongo wake.
Afisa Lishe aliongeza kuwa Mtoto kuwa na uzito usioendana na umri pia ni utapiamlo uliosababishwa na mtoto kukosa madini na vitamini hali ambayo hupelekea mtoto dumaa ubongo.
“ watoto wengi walioshindwa kuwa na kimo kulingana na umri wao wanashida ya kuto elewa, kufikiri na kujifunza mambo kwa wepesi hasa wakiwa shuleni kutokana na uwezo wao wa kuelewa kuwa chini sana hali inayopelekea walimu kutumia nguvu nyingi kufundisha bila mafanikio yaliyotarajiwa”,anasema Ngatunga.
Ili kuwa na kizazi cheye watu wenye uwezo mzuri wa kufiri , kujifunza na kujiamini ni lazima mama mjamzito azingatie lishe bora, kupata huduma za afya kwa kwenda kliniki, kunyonyesha mtoto kwa muda wa miaka miwili na kumupa lishe inayotakiwa.
Ifike wakati jamii ichukue hatua ili kuwasaidia watoto kukua vizuri kimwili na kiakili ikiwa pamoja na kuhakikisha Taifa linaendelea kwani udumavu kwa watoto unarudisha nyuma maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Aidha wanawake wanapaswa kufuata taratibu za kiafya zinazotolewa na wataalam wa afya ili kuwapa watoto kinachostahili ikiwa ni njia bora ya kuepuka tatizo la udumavu linalowakuta watoto wengi nchini na kusababisha kurudisha nyuma maendeleo yao ya kimwili na kiakili, kumaliza tatizo la udumavu katika jamii inawezekana chukua hatua ya kuzingatia lishe bora na huduma za afya
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa