Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi kupitia mkutano maalum wa Baraza la Madiwani uliofanyika mnamo tarehe 28 Septemba, 2021 katika ukumbi wa mikutano ulioko Mbuyuni kwa kauli moja wameridhia kupokea na kupitisha taarifa ya kufungwa kwa hesabu za Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2021.
Kaimu Mweka hazina, Bw. Athumani Jumanne alisema kwa mujibu wa kifungu Na. 40 cha sheria ya fedha za Serikali za Mitaa ya mwaka 1982, (The Local Government Finance Act, 1982) pamoja na agizo katika kanuni za Fedha za Serikali za Mitaa Na. 31 (The Local Authority Financial Memorandum of 2009) zinaelekeza Halmashauri zote nchini kufunga mahesabu yake ya mwaka mwisho wa mwaka na kuyawasilisha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kabla au ifikapo tarehe 30 Septemba ya kila mwaka.
Kaimu Mweka hazina aliendelea kuwaelezea wajumbe wa mkutano huo kuwa kwa mujibu wa Kanuni/Muongozo wa Fedha za Serikali za Mitaa (LAFM) 2019 Na. 31 (7), taarifa ya mahesabu hayo yaliyofungwa yanapaswa kuwasilishwa katika kamati ya Fedha, Utawala na Mipango na Baraza la Madiwani kwa ajili ya kujadiliwa na kupitishwa ndipo hesabu hizo ziwasilishwe kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Aliendelea kusema kaimu mweka hazina, hesabu za Halmashauri za kuishia Juni, 2021 zimefungwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya utayarishaji wa hesabu za umma yaani International Public Sector Accounting Standards (IPSAS Accrual) pamoja na kanuni za Fedha za Serikali za Mitaa (Local Government Financial Memorandum (LGFM)), 2009 na Local Authority Accounting Manual (LAAM), 2009.
Halmashauri ilimaliza mwaka wa fedha 2020/2021 tarehe 30 Juni, 2021 ikiwa na albaki ya jumla ya Sh. 2,693,633,061 katika akaunti zake za BoT na NMB pamoja na akaunti za shule, vituo vya afya, zahanati na vijiji. Pia kulingana na 'Statement of Financial Performance' taarifa ya mwenendo wa fedha kwa kuzingatia viwango vya kimataifa vya utayarishaji wa hesabu (IPSAS Accrual) mapato yalifikia Sh. 30,291,801,646 na matumizi 22,093,419,070 hivyo kufanya ziada (Surplus) ya Sh. 8,198,382,576 kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni, 2021.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa