Kukamilika kwa Mradi wa Maji Chipingo – Mkaliwata unaotarajia kuhudumia wananchi wa vijiji 8 katika kata za Chikoropola na Mnavira sio tu utamtua mama ndoo kichwani lakini pia utamaliza tatizo la vifo vinavyosababishwa na mamba katika mto Ruvuma wakati wananchi hao wakiwa wanachota maji.
Hayo yamezungumzwa na waziri wa maji Profesa Makame Mbarawa wakati wa ziara ya kuKagua miradi ya maji inayoendelea kutekelezwa sasa wilayani Masasi na kueleza kuwa serikali inatumia fedha nyingi sana kutekeleza miradi ya maji lengo ikiwa ni kuwaondolea shida ya maji wananchi wa maeneo yote mijini na vijijini.
“Mradi wa Chipingo –Mkaliwata ni mradi maalum kutokana na umuhimu wake kwa wananchi kwani utaondoa matatizo mawili ya ukosefu wa maji lakini pia vifo na ulemavu wa kudumu unavyosababishwa na mamba wa Mto Ruvuma pindi wananchi wanapochota maji katika mto huu, nakuagiza mkandarasi ufanye kazi usiku wa mchana ili mradi ukamilike haraka” alisema Mbarawa.
Prof: Mkame alieleza kuwa serikali ina fedha za kutosha za kutekeleza miradi ya maji ambayo inaendelea na mipya ili kufikia lengo la vijiji vyote kuwa na huduma ya maji ifikapo mwaka 2020.
“Naomba niwahakikishie kuwa mwezi desemba mtapata maji na kero ya maji itakuwa imeisha kabisa, nitamsimamia mkandarasi kuhakikisha anamaliza kazi ndani ya kipindi akishindwa nitamfukuza kwani haiwezi kuwavumilia wakandarasi wasioweza kwenda na kasi inayotakiwa” alisisitiza Prof Makame
Wananchi wanapaswa kutumia muda wao mwingi kufanya shughuli za maendeleo na sio kukesha kutafuta huduma ya maji, hivyo serikali itahakikisha mradi huu unakamilika desemba 2018 ili wananchi wa chikolopola na Mnavira waepukane na adha ya kufuta maji mto Ruvuma ambako kuna mamba wanaohatarisha maisha yao.
Aidha mheshimiwa Makame Mbarawa alitumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi kutunza miundombinu ya maji kwani serikali inatumia fedh nyingi sana kuweka miundombinu hiyo, lakini pia utunzaji wa vyanzo vya maji ni muhimu sana wani bila kutunza vyanzo vya maji hakutakuwa na maji.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Chikolopola Mheshimiwa Edward Mahelela alimweleza Waziri kuwa zaidi ya watu 30 akiwemo watoto wameuawa na mamba wakati wengine wakipata ulemavu wa kudumu, hivyo kukamilika kwa mradi huo utaondoa kero zote mbili kwa wakati mmoja.
Mhandisi wa maji wa halamashauri ya wilaya ya amasasi Ndugu Fransis Bwire, akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo alieleza kuwa mradi huo utagharimu shilingi 3,983,700,074.22 mpaka kukamilika kwake.
Mhandisi alieleza kuwa vijiji vitakavyonufaika na mradi huo ni Chipingo, Manyuli,Rahaleo,Mapili, Chikolopola, Mkaliwata, Namyomyo na Mnavira vijiji ambapo kwa sasa wanatumia maji ya Mto Ruvuma pamoja na kununua wa bei kubwa ambapo ndoo moja inauzwa kati ya 500 hadi 1000.
Mradi wa chipingo –mkaliwata ni kati ya miradi ya miradi 6 ya maji ambayo inatekelezwa na halamashauri ya wilya ya masasi kupitia Programu ya maji na usafi wa mazingira vijijini (RWSSP).
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa