Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa ndugu Amour Hamad Amour ameipongeza halmashauri ya wilaya ya masasi mkoani mtwara na wananchi wake kwa kuwa na miradi mizuri na yenye ubora wa hali ya juu inayolengo kukudumia wananchi hali inayoipa heshima serikali kwa wananchi wake.
Hayo aliyazungumza wakati wa kukagua na kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa wodi la akina mama na watoto katika Kituo cha Afya cha Chiwale ambapo alisema serikali ya awamu ya tano imedhamiria kusogeza karibu huduma za afya, elimu na huduma nyingine kwa wananchi
Amour alisema kuwa, Ubora wa miradi unategemea na usimamizi imara, ushirikishwaji wa wananchi na uchaguzi bora wa wakanadarasi wanaojenga miradi kwa kuzingatia mikataba ya ujenzi
Amour alifafanua kuwa serikali inahitaji wakandarasi ambao wanafanya kazi kwa viwango na kumaliza kazi kwa wakati ili serikali iweze kutimiza adhima yake ya kuwahudumia wananchi kwa wakati na si vinginevyo. Na kuongeza kuwa wakanadarasi kama huyo ndio wanaostahili kupata kazi mbalimbali za ujenzi kwani wanajenga kwa kulingana na thamani ya fedha.
“ Mimi nimeridhishwa na ujenzi huu kwa asilimia mia moja kuanzia muundo wake na ujenzi kwa ujumla uko kwenye viwango stahiki niamuomba akamilishe kwa viwango hivi ili kiongozi atakayekuja kufungua jengo hii alikute likiwa kwenye ubora wa juu zaidi” alieleza Amour.
Aidha Amour aliwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili jengo hilo liweze kukamilika na hatimaye wakinamama wawe na mahali pazuri pa kupata huduma za afya kwa akina mama wajawazito, wanaotarajia kujifungua, waliofanyiwa upasuaji na watoto waliozaliwa na uzito mdogo.
Mradi huo ulianza mwezi januari 2017 na unatarajia kukamilika mwaka 2017.
Zahanati ya chiwale inahudumia wananchi 17,770 ambapo wanaume 7855 na wananwake 9915 kutoka vijiji 3 vya chiwale, ufukoni, Mkwapa na vijiji vingine vya kata jirani.
Mwenge wa uhuru ukiwa masasi ulitembelea jumla ya miradi mitano (5) yenye thamani ya zaidi ya shilingi biolioni mbili.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa