• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE KITAIFA 2018,APONGEZA UTEKELEZAJI WA MIRADI HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI

Posted on: June 14th, 2018

Serikali  ya awamu ya tano imedhamiria kuwekeza katika miundombinu ya katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu afya na maji kwa kutoa fedha za utelelezaji wa miradi hiyo, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imeweza kutekeleza miradi yake kwa kuzingatia viwango na ubora unaotakiwa, hali ambayo  imeshawishi mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2018 kuridhia kuweka mawe ya msingi katika miradi yote, hongereni sana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Bi Changwa M. Mkwazu akipokea Mwenge wa Uhuru eneo la mapokezi kijiji cha Mpeta tarehe 13.06.2018

Pongezi hizo zilitolewa na kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndugu Charles Francis Kabeho wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri hiyo zilizofanyika tarehe 13 juni,2018 na kueleza kuwa Halmashauri ya wilaya ya masasi imekuwa na miradi ambayo imetekelezwa kwa viwango na ubora wa hali ya juu hivyo wanastahili pongezi kubwa sana.

Wakimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa wakiongozwa  Ndugu Charles Francis Kabeho (wa tatu kutoka kulia) wakati wa mbio za mwenge wa Uhuru Halmashauri ya Wilaya ya masasi 13 juni 2018

“Utekelezaji wa miradi kwa kutumia  fedha za serikali au nguvu za wananchi lazima  uzingatie ubora na thamani ikiwemo matumizi ya matofali yenye viwango na utaalamu stahiki, Halmashauri ya wilaya ya masasi imeonyesha ubora huo kwenye miradi yake yote ndio maana Mwenge wa Uhuru umeridhia kuweka mawe ya msingi “ alisema kabeho.

Mkimbiza Mwenge wa Uhuru   Ndugu Charles Francis Kabeho (aliyavaa skafu) wakati baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa madarasa matatu shule ya msingi Mnavira tarehe 13.06.2018

Aidha Kabeho amewapongeza viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi akiwemo Mkuu wa Wilaya, Viongozi wa Chama Tawala, Mwenyekiti wa Halmashauri, Mkurugenzi Mtendaji, Wahehimiwa Madiwani, Watendaji na Wananchi wote kwa ushirikano walio nao katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo katika kuwahudumia wananchi.

“Kwa utekelezaji huu ningependa kuziambia Halmashauri zingine kuja kujifunza katika Halmashauri hii kwani utekelezaji wa miradi upo katika viwango vya juu sana lakini pia wameweza kubakiza fedha na kuweza kujenga miundombinu mingine” alisema kabeho.

Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wakipokea Mwenge wa Uhuru 

Katika kutekeleza Ujumbe wa Mwenge wa Uhuru unasema Elimu ni Ufunguo wa Maisha, Wekeza Sasa, Kabeho ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa kuwa na mpango wa utoaji wa chakula kwa wananfunzi shuleni ambapo wazazi wameonyesha kutambua wajibu wao wa kuhakikisha watoto wanapata chakula wakiwa shule hali ambayo inataongeza ari kwa wananfunzi kujisomea na hatimaye kuongeza ufaulu.

Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa   Ndugu Charles Francis Kabeho akizindua mpango wa kutoa chakula katika shule ya sekondari Namwombwe

Kwa upande wa vikundi ya wanawake na vijana, Kabeho ameipongeza Halmashauri kwa kufanikiwa  kutoa mikopo kwa vikundi  41 wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru yenye thamani ya shilingi milioni 144,219,000 kwani serikali inataka wanawake na vijana kushiriki kwa vitendo katika kufikia tanazania ya viwanda kwa kuanzisha viwanda vidogovidongo na vya kati.

Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa   Ndugu Charles Francis Kabeho akitoa hundi za mikopo kwa vikundi vya wananwake na vijana

Kufuatia ongezi hizo, Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Selemani Mzee amewashukuru Watendaji na Viongozi wa Halmashauri hiyo kwa umoja na mshikamo walionao katika kutekeleza shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu kwani kutokana na ushirikiano wao wamefanikiwa kupata pongeza katika utekelezaji wa miradi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi bi Changwa M.Mkwazu (aliyeshika karatasi) akiwa katika picha ya pamoaja na baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo wakifurahia ujio wa mwenge wa uhuru katika Halmashauri yao.

Mbio za mwenge wa uhuru katika halmashauri ya wilaya ya masasi  zimeweza kuweka mawe ya msingi katika miradi minne(4) kutoa hundi kwa vikundi vya wananwake na vijana na kuzindua clabu ya wapinga Rushwa shule ya sekondari Namombwe yenye  thamani ya shilingi shilingi  bilioni 2,406,699,000

Mkimbiza Mwenge wa Uhuru Kitaifa   Ndugu Charles Francis Kabeho akiwa kwenye ukaguzi wa mradi wa ujenzi shule ya wasichana ndwika

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • WATENDAJI WA SERIKALI TEKELEZENI WAJIBU WENU WA KIKAZI,MSIJIHUSISHE NA MAMBO YA SIASA: BARAZA LA MADIWANI

    May 15, 2025
  • WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI NA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO ILI KUFANIKISHA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA AWAMU YA PILI.

    May 15, 2025
  • WATAALAMU MASASI DC WAPATIWA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO WA UJIBUJI HOJA ZA CAG.

    May 11, 2025
  • KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO ROBO YA III (JAN -MACHI 2025) INAYOTEKELEZWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI.

    May 06, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa