WADAU wa sekta ya elimu wilayani Masasi mkoani Mtwara wameshauri kuongeza kasi ya kuwa na ushirikiano wa pamoja katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta hiyo ili kuweza kufanikisha lengo la kuinua kiwango cha elimu wilayani Masasi.
Aidha,wadau hao wamezitaja baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa ni moja ya sababu inayochangia kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani Masasi kuwa ni walimu kutokuwa na hari ya ufundishaji, wazazi na walezi kutothamini thamani ya elimu,watendaji wa idara ya elimu kutokuwa na ushirikiano wa karibu na walimu.
Ushauri huo waliutoa jana kwenye kikao cha pamoja cha wadau wa elimu wilayani Masasi kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya Masasi na kuhudhuriwa na makundi mbalimbali ambao ni wadau wa sekta hiyo ambao ni walimuwakuu wa shule za sekondari na msingi,watendaji wa kata,maafisa elimu msingi na sekondari,waratibu kata elimu,wakuu wa idara,walimu wastaafu,viongozi wa dinina wazee maarufu.
Walisema moja ya sababu ambayo inayochangia kushuka kwa kiwango cha elimu wilayani Masasi ni kukosekana kwa ushirikiano wa pamoja baina ya wadau wenyewe wa elimu katika kupanga na kutekeleza mikakati na maazimio yanayowekwa kwenye sekta ya elimu wilayani humo na kwamba kila mmoja hufanya anavyotakahali inayopeleka kutokuwa na makakati wa pamoja na kusababisha elimu kushuka.
Wameeleza kuwa wazazi na walezi pia wanatakiwa kutambua kwamba na wao ni wadau wakubwa wa sekta ya elimu hivyo lazima waone umuhimu wa kuchangia elimu kwa ajili ya watoto wao kwani urithi wa mtoto ni elimu na badala ya kufikiri kuwa kila kitu kinapaswa kufanya na serikali peke yake.
Wadau hao walisema ni wakati muafaka sasa kkuanza kujitathimini na kuwa kitu kimoja kwa kushirikiana kwa ukaribu ili kuweza kuzitatua changamoto hizo na hatimaye kuwa katika ramani nzuri ya kitaaluma kama ilivyo kwa wilaya nyingine nchini badala ya kuendelea kushika mkia na kunyoosheana vidole.
Walisema wilaya ya Masasi kupitia halmashauri zake mbili ya wilaya na ile ya mji Masasi kwa miaka ya hivi karibuni 2016 pamoja na mwaka 2017 zimekuwa hazifanyi vizuri katika sekta ya elimu kuanzia shule za msingi na sekondari hasa katika matokeo ya darasa la saba pamoja na kidato cha nne kuanzia ngazi ya wilaya,mkoa na taifa.
Akichangia mada katika kikao hicho mwalimu wa shule ya msingi Mkomoindo,Joseph Chikawe alisema watendaji wa idara ya elimu pamoja na uongozi wa serikali ya wilaya wana wajibu wa kukutana na walimu kwa njia nyingine ili walimu hao waweze kueleza kero zao ambazo zinawafanya wasiwe na hari ya kujituma katika ufundishaji kwenye shule zao.
“Walimuwana kero nyingi sana ndani ya nafsi zao ambazo kero hizi ni moja ya sababu inayowafanyawashindwe kuwa na morali ya kazi kwenye shule zao, hapa kamwe hawawezi kuzisema kwa sababu wakuu wa idara wapo lakini kama uongozi wa serikali na wakuu waidara hao tukikutana pamoja tutaweza kuzisema wazi,”alisema.
Akifungua kikao hicho mkuu wa wilaya ya Masasi, Selemani Mzee alisema bado watendaji wa idara ya elimu wilaya humo wanayo kazi kubwa ya kufanya ilikuhakikisha sekta ya elimu inaondokana na changamoto zinazoikabili sekta hiyo na kusababisha kushuka kwa kiwango cha elimu.
Mzee alisema serikali itaendelea kuisimamia sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuwashawishi wadau wa elimu kuweza kuachangia masuala mbalimbali katika elimu ili elimu iweze kuthaminiwa na kuwa katika matokeo mazuri.
Kwa upande wake afisa ukaguzi wa shule za msingi na sekondari wilayani Masasi aliomba halmashauri kutenga fedha na kuzitoa kwa idara ya ukaguziili iweze kufanya shughuli za ukaguzi kwa ufanisi zaidi ukilinganisha na hivisasa ambapo kitengo hicho kinafanya kazi katika mazingira magumu.
Kwa pamoja wakurugenzi wa halmashauri hizo mbili, halmashauri ya wilaya na ya mji , Bi. Changwa Mkwanzu na Bi. Gimbana Ntavyo walisema wao kama wakurugenzi wamezipokea changamoto na ushauri uliotolewa na wadau hao hivyo kama wao ni wasimamizi wa halmashauri hizo wanaahidi kuzifanyia kazi kwa nguvu moja ili kurudisha hali ya kitaaluma wilayani humo ambayo kwa sasa imeshuka kwa kasi.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa