Kanisa la anglikani dayosisi ya masasi limefanikiwa kumtuma mama wa namajani katika halamashauri ya wilaya ya masasi ndoo kichwani baada ya kuchimba kisima cha maji katika kijiji hicho na hivyo kuwapa fursa ya kutumia muda wao kufanya shughuli za mandeleo.
Akikabidhi mradi huo wa kisima kwa wananchi wa kijiji cha Namajani na mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya masasi hiyo Changwa M Mkwazu Mwashamu Askofu wa kanisa la Anglikani dayosisi ya masasi James B. Almasi aliwataka wanawake na wananchi kutumia maji hayo bila kujali tofauti zao zikiwemo za kidini kwani mradi huo ni wa wananchi wote,
Askofu Almasi alisema kuwa mradi huu umegharimujumla ya shilingi milioni kumi na mbili (12,000,000) kuanzia hatua ya upembuzi mpaka uchimbaji na matengenezo yote.
Askofu Almasasi alisema kuwa kanisa limeamua kuchimba kisima cha maji kwa ajili ya wananchi wote na sio wakristo kwani kanisa halilengi kuhudumia waumini wake tu bali ni watu wote kama ilivyo kwenye huduma za shule na zahanati.
“Maji haya ni haya sio ya wakisto ni ya watu wote sitegemei huduma hii ya maji ilete mifarakano kwa wananchi bali ilete umoja” alisema Askofu Almasasi
Aidha askofu Almsi alisema kuwa kanisa liliamua kuchimba kisima cha maji kutokana na tatizo la maji katika ukanda wa magharibi kuwa kubwa sana kwani wananchi walikuwa wanatumia muda mwingi kutafuta maji badala ya kufanya shughuli za maendeleo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Chwangwa M. Mkwazu alimshukuru Askofu Almas kwa jitihada za kanisa hizo kuamua kuchimba kisima cha maji katika kijiji cha Namajani kwani kitawasaidia wananchi kuata huduma ya maji kwa ukaribu zaidi tofauti na hapo awali ambapo iliwalazimu kufuata maji mbali.
Mkwazu alisema kuwa serikali imedhamilia kumtua mama ndoo kichwani kwa kumsogezea huduma ya maji hivyo kanisa la Anglikani masasi limesaidia kutimiza adhima ya serikali kwa kuchimba kisima katika kijiji hiki ambacho kinashida kubwa ya maji.
Aidha Mkwazu aliwaeleza wananchi kuwa baada ya kukabidhiwa mardi huo kijiji kitaunda jumuiya ya watumia maji ili waweze kuwa na utaratibu mzuri wa kuuza maji na hatimae kupata mapato ya kuweza kufanya matengenezo ya mradi yatakapotokea.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa