Kamati ya Fedha Halmashauri ya Wilaya Masasi Mkoani Mtwara tarehe 06/05/2024 imefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo inatekelezwa ndani ya Halmashauri hiyo.
Kamati hiyo ikiwa Katika Jimbo la Lulindi imekagua ujenzi wa matundu 23 ya vyoo Katika Shule ya Msingi Ng'uni iliyopo katika Kata ya Sindano, ikiwa ni mradi wa SWASH unaogharimu kiasi Cha Fedha shilingi 51,858,872.00.
Mradi huo ambao kwasasa upo katika hatua ya umaliziaji kwa kufunga mfumo wa Maji, Kupaka rangi, Kupachika Milango, kuweka Tiles, kutengeneza Eneo la kunawia mikono kwa Wanafunzi, Waalimu,na wafanyakazi wengine, Kutengeneza rapu Pamoja na ngazi, inaelezwa kuwa utakapokamilika utaboresha sana Afya za Wanafunzi, Utajenga hali ya kujiamini kwa Wanafunzi hasa wa kike waliopo kwenye Makuzi na kupunguza utoro.
Kwaupande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Masasi Ndug.Ibrahimu Chiputula ameutaka uongozi wa Shule na kamati inayosimamia ujenzi huo kuhakikisha unajengwa kwa viwango vinavyotakiwa na uwe wa mfano kulingana na thamani ya fedha zilizotolewa na pia ifikapo tarehe 30/05/2024 mradi huo uwe umekamilka.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa