Kamati ya Fedha utawala na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya Masasi Jana Tarehe 24/07/2024 katika muendelezo wa ziara yake ya kutembelea, kukagua na kupata taarifa juu ya miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo inatekelezwa katika Halmashauri hiyo imete mbelea mradi wa ujenzi wa madarasa mawili na Ofisi Katika Shule shikizi ya Nangwale iliyopo katika Kata ya Namwanga Jimbo la Lulindi Halmashauri ya Wilaya Masasi.
Ujenzi huo ulianza rasmi mnamo mwaka 2021 kupitia nguvu za Wananchi hadi hatua ya Renta june 2023 ulihusisha ujenzi wa boma la madarasa 2 na Ofisi Moja ya walimu.
Hata hivyo kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake ndg.Ibrahimu Chiputula ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, imeonyesha kuridhishwa na nanna mradi huo ulivyotekelezwa kwa viwango vya hali ya juu ukilinganisha na thamani ya fedha iliyopokelewa.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tofauti wajumbe wa Kamati hiyo mbele ya Wananchi waliojitokeza na kuungana nao nakuwapa fursa kusikiliza taarifa ya mradi huo wamesema kwa Pamoja wanawapongeza Sana wananchi wote wa kitongoji hicho kwa kuonyesha moyo wa kujitolea na hatmaye kufanikisha mradi huo ambao utakwenda kutatua changamoto ya Shule kwenye eneo lao.
Wamesema " tunawapongeza sana tena Sana,mmejitoa na kuamua kushirikiana na Diwani wenu wa kata hii ya Namwanga na kuona kitongoji hiki kinakuwa na Shule yake, Sasa matumaini yetu shule hii si tu ibaki kuwa shikizi hapana tunataka kuona madarasa mengine yanaongezwa haraka sanjali na ujenzi wa matundu ya vyoo ili shule hii iwe shule kamili ambayo itahudumia Watoto wenu na vijiji jirani pia Watoto wao watakuja kupata Elimu hapa,kwaiyo hongereni sana na endeleeni kumpatia ushirikiano Diwani wenu ili mpate Maendeleo mengine katika nyanja mbalimbali."
Aidha ujenzi wa mradi huo wa madarasa mawili na Ofisi ya walimu katika Shule shikizi Nangwale zilipokelewa fedha kwa awamu mbili ambapo katika awamu ya Kwanza mnamo tarehe 01/07/2023 walipokea shilingi 10,000,000/,= na awamu ya pili tarehe 11/03/2024 walipokea Fedha shilingi 15,000,000/= na kufanya jumla ya Tshs.milioni 25,000,000/= kutoka Halmashauri fedha za mapato ya ndani ili kumalizia ujenzi wa madarasa mawili na Ofisi ya walimu ambapo wamefanikiwa kukamilisha Kwa ujenzi wa gebo 2, kumwaga jamvi, kupaua Jengo lote, kupiga plasta, na puchi kwa nyuma na mbele.
Kazi zingine ni kufunga blandering, kufunga gypsum board na kuskim, kupaka rangi ndani na nje, kuweka tile's pamoja na malipo ya mafundi wa ujenzi huo.
... @ Masasi DC
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa