Kamati ya fedha Halmashauri ya Wilaya Masasi imekagua mradi wa umaliziaji wa chumba kimoja Cha Maabara katika Shule ya Sekondari Sindano.
Mradi huu ni wa SEQUIP ambapo Mwezi Dec 2023 kiasi Cha Fedha shilingi milioni 30,000,000.00. kilipokelewa kutoka Serikali kuu kwa ajili ya ukarabati wa chumba kimoja Cha Maabara ya Kemia.
Ibrahimu Chiputula ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Masasi, baada ya kukagua mradi huo ameonyesha kutoridhishwa na hali ya utekelezaji wa mradi huo ambapo wamebaini Kuna uzembe unafanyika ambao unachelewesha kukamilika kwa wakati mradi huo.
Amesema" huu mradi mnatuchanganya sana, yaani hadi kufikia sasa hivi inaonekana huu mradi bado haujaisha wakati mmepatiwa muda mrefu shilingi milinioni 30"?..aliuliza
Hata hivyo kutokana na changamoto hizo Kamati ya fedha imeiagiza Kamati inayosimamia ujenzi wa mradi huo kuhakikisha wanafanya kila iwezekanavyo wanakamilisha ukarabati wa Maabara hiyo haraka na ikiwemo uwekaji wa Milango inayotakiwa mara ifikapo tarehe 30/05/2024, kabla Kamati hiyo ya fedha haijarudi tena shuleni hapo ifikapo june mosi mwaka huu.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa