Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa ndugu Charles Francis Kabeho amezipongeza Wilaya za Mkoa wa Mtwara zilizofanya vizuri katika mbio za mwenge wa uhuru 2018 zilizoanza tarehe 11 juni na kumalizika tarehe 19 juni 2018 ambapo amesema kuwa baadhi ya wilaya zilikuwa na miradi mizuri ambayo mwenge wa uhuru uliweza kupitia bila matatizo.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mhe Gelasius Byakanwa (mwenye shati la kitenge) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Lindi mhe Godfrey Zambi leo tarehe 20.06.2018 katika viwanja vya shule ya msingi Madangwa
Kabeho ametoa pongezi hizo leo wakati wa makabidhiano ya mwenge wa uhuru kati ya mkoa wa mtwara na lindi yaliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Madangwa mkoani Lindi na kueleza kuwa wakati wa ukaguzi wa miradi kuna baadhi ya wilaya zimefanya vizuri sana kwa kuwa na miradi mizuri iliyozingatia thamani ya fedha na ubora unaotakiwa hivyo zinastahili pongezi.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mhe Gelasius Byakanwa (aliyeshika mike) akifurahia jambo wakati kukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Lindi leo tarehe 20.06.2018 katika viwanja vya shule ya msingi Madangwa
Aidha, Kabeho ameeleza kuwa, kwa wilaya ambazo miradi yake imekutwa na dosari nazo nazipongeza kwa kazi walizofanya na kutokana na dosari hizo wanaweza kurekebisha na kujifunza namna bora ya kusimamia miradi ya maendeleo kwa kuzingatia viwango stahiki.
Akisoma taarifa ya Mkoa wakati wa makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru mbele ya kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa ndugu Charles Francis Kabeho, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa amesema kwa upande wa Halmashauri zilizopatikana na dosari kwenye miradi yao ameunda kamati ya uchunguzi ili kubaini chanzo na mapungufu yaliyojitokeza kwenye miradi hiyo iliyokataliwa na kushauri hatua gani zichuliwe kwa mujibu wa sheria.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mhe Gelasius Byakanwa (aliyeshika karatasi ) akisoma taarifa wakati wa kukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Lindi leo tarehe 20.06.2018 katika viwanja vya shule ya msingi Madangwa
Byakanwa amefafanua kuwa mwenge wa uhuru ukiwa Mtwara umepitia miradi 76 katika sekta ya elimu, afya,maji,barabara,utawala bora na maendeleo ya wanawake na vijana ambapo kati ya hiyo miradi 24 imewekewa mawe ya msingi, 10 imefunguliwa, 11 imezinduliwa, 27 imeonwa na kukaguliwa na miradi 4 imekataliwa yenye thamani ya shilingi milioni 634,286,920 sawa na asilimia 2.14 ya gharama za miradi yote shilingi 29,661,235,832.
Watumishi na viongozi wa Mkoa wa Mtwara wakiwa tayari kukabidhi mwenge wa uhuru Mkoa wa Lindi
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa