HUDUMA ZA UPASUAJI KWENYE VITUO VYA AFYA KUPUNGUZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara ndugu Bw. Alphayo Kidata ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa kuweza kuanza kutoa huduma za upasuaji kwa akinamama wajawazito zaidi ya 20 wanaopata changamoto mbalimbali wakati wa kujifungua katika kituo cha afya nagaga.
Kidata alieleza hayo wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kujionea utekelezaji wa ujenzi wa miundombinu ya vituo vya afya vya Nagaga na Chiungutwa pamoja na hospitali ya Halmashauri inayojengwa katika kata ya mbuyuni ambayo imegharimu shilingi bilioni 2.3
Katibu Tawala wa Mkoa wa Mtwara ndugu Bw. Alphayo Kidata(aliyevaa kofia) akipata maelezo kutoka kwa mkuu we kitengo cha Upasuaji katika kituo cha afya Cha Nagaga.
“Kituo cha afya Nagaga ni kati ya vituo vya afya 6 vilivyonza kutoa huduma kwa wananchi kati ya vituo 11 vilivyojegwa mkoa wa mtwara ni jambo la kujivunia sana kwani wananchi wanataka huduma na sio kuona majengo tu” alieleza Kidata.
Kidata ameeleza kuwa “Hii ni hatua kubwa sana katika kuhakikisha tunapunguza vifo vya akinamama na watoto wachanga wakati wa kujifungua na haya ndio madhumuni ya Mhe Rais katika kuhakiksha huduma za afya zinawanufaisha wananchi”
Aidha Kidata amelidhika na ubora wa majengo na kueleza kuwa ubora wake unaendana na thamani ya fedha iliyotolewa“ nimefarijika kuona majengo yenye ubora wa juu na yaliyomaliziwa vizuri, kwa ujenzi huu majengo haya yatadumu kwa muda mrefu sana hongereni sana”
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa