Halmashauri za Mikoa ya Lindi na Mtwara zasisitizwa kuwa na bidhaa na vipando bora na vyenye tija vya mazao mabalimbali kwenye mabanda yao vinavyozingatia kanuni bora za kilimo cha kisasa ili kufanyika darasa kwa wakulima na wafugaji wakati wa maonesho ya nanenane yatakayofanyika kitaifa katika kanda ya kusini viwanja vya ngongo mkoani lindi mwezi wa nane mwaka huu.
Msisitizo huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe Godfrey W. Zambi leo wakati wa kikao cha maandalizi ya maonesho hayo kilichohusisha wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wenyeviti na wakurugenzi wa Halmashauri za Mikoa ya Lindi na Mtwara pamoja na wadau wengine wa maendeleo lengo ikiwa ni kufanya maandalilizi ya maonesho hayo ambayo yanafanyika kitaifa mara ya nne mfululizo katika kanda ya kusini.
Zambi aliwaeleza wajumbe kuwa maonesho hayo yanapaswa kuwa darasa kwa wakulima na wafugaji pamoja na wananchi kwa ujumla kwani maonesho hayo yanalenga kutoa elimu juu ya kilimo cha kisasa na chenye tija kwa vitendo na ili wakulima wakaweze kutumia utaalamu huo katika maeneo yao na hatimaye kuongeza uzalishaji utakaopelekea kufikia uchumi wa kati.
Upelekaji wa utaalamu wa kilimo, mifugo na uvuvi pamoja na bidhaa mbalimbali kwa wananchi unatakiwa kuwa uwe wenye tija hivyo kila banda linatakiwa liwe na vipando vinavyoonesha uzalisha bora kama kaulimbiu ya maonesho ya nanenane mwaka huu 2017 inayosema “ zalisha kwa tija mazao na bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati” alisema Mhe Zambi.
Mhe Zambi alisistiza kuwa “Vipando vyetu na bidhaa kwenye mabanda yetu lazima vionyeshe tija, kama ni korosho, alizeti, ufuta na zao lolote lile ioneshe kama mkulima atazalisha namna iliyo kwenye vipando vyetu atazaliza kwa wingi na kwa ubora wa unaotakiwa katika ushindani wa soko la zao hilo”
Halmashauri zikakikishe zinazimamamia vipando ili mpaka kufiki wakati wa maonesho eneo hilo kweli lionekane ni sehemu ya watu kujifunza kwa vitendo kwa kuona mazao ya aina mbalimbali yakiwa yamestawi vizuri ili washawishike kwenda kutumia teknologia hizo katika shughuli zao za kilimo na hivyo kuongeza uzalishaji kwa wakulima na hatimaye kufikia uchumi wa kati kama serikali ya awamu ya Tano inavyosisitiza kuwa ifikapo 2025 Tanzania iwe imefikia uchumi wa kati.
Aidha Mhe. Zambi amewaeleza wajumbe kuwa maonesho ya nanenane kitaifa kwa kanda ya kusini yatafanyika kwa mara ya mwisho mwaka huu wa 2017 kufuatia maelekezo yalitolewa na wizara kuwa maonesho hayo kitaifa itabidi yapelekwe kanda zingine, hivyo mwakani maonesho haya yatafanyika kikanda kama ilivyokuwa kwa maeneo mengine.
Kwa kanda ya kusini maonesho ya nanenane kitaifa yalianza mwaka 2014 na yataishia mwaka huu wa 2017 ambapo yamefanyika mfululio kwa muda wa miaka minne.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa