Halmashauri ya Wilaya Masasi Mkoani Mtwara Leo julai 31/07/2024 imewasilisha taarifa ya utendaji wa kazi wa Halmashauri kwa kipindi cha Mwaka wa fedha 2023/2024 huku taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ikiwakonga nyoyo waheshimiwa Madiwani ambapo inaonyesha Halmashauri imefanikiwa kukusanya kiasi Cha Fedha shilingi Bilioni 4.796 sawa na asilimia 104.8%
Akiwasilisha taarifa hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Bi.Beatrice Mwinuka mbele ya baraza la Madiwani Katikati mkutano mkuu wa kufunga mwaka, Afisa Mipango wa Halmashauri hiyo Bw. Nelson John amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024, Halmashauri imeidhinishiwa bajeti ya kukusanya/kupokea Jumla ya shilingi Bilioni 40,644,138,368.00 ambapo Kati ya fedha hizo sh.4,578,988,000.00 ni mapato vyanzo vya ndani, na kiasi cha Shilingi 21,917,396,000,00 ni ruzuku kwa ajili ya kulipia mishahara, shilingi 1,203,928,000,00 fedha za ruzuku kwa ajili ya matumizi mengine, shilingi 5,294,385,367.81 michango kutoka kwa wadau wa Maendeleo (wahisani) na shilingi 7,649,441,000.00 ni fedha za ruzuku za miradi ya Maendeleo Kutoka Serikali kuu.
Amesema hata hivyo ukijumuisha na bakaa ya Mwaka 2023/2024 ya Shilingi 339,565,379.06 kufanya bajeti kuu inayotekelezwa kwa Mwaka 2023/2024 kufikia jumla ya shilingi Bilioni 40,987,703,746.87
Bw. Nelson katika taarifa hiyo ameendelea kuelezea kuwa katika kipindi Cha Mwezi julai 2023 hadi Juni 2024 Halmashauri ilijiwekea lengo la kukusanya mapato ya shilingi Bilioni 4,578,988,000.00. ambapo Kwa kipindi Cha Mwezi Juni pekee 2024 Halmashauri imeweza kukusanya kiasi cha Shilingi Milioni 429,522,309.52 na hivyo kufanya Jumla ya mapato yote katika vyanzo vya mapato ya ndani kufikia shilingi bilioni 4,796,609,248.99 sawa na asilimia 104.8% na kufanya kuvuka lengo la mwaka wa fedha, ambapo ongezeko la makusanyo hayo kwa mwaka wa fedha 2023/24 ni Shilingi Milioni 217,621,248.
Aidha Pamoja na kuainisha baadhi ya vyanzo hivyo vya mapato Kama vile ushuru wa mazao kama ufuta, korosho, mahindi,mbaazi, ushuru wa leseni za biashara, ada za ukaguzi na vibali vya ujenzi, leseni za biashara n.k pia ameongeza kuwa yapo mapokezi ya fedha kwa ajili ya Shughuli za maendeleo ambapo katika kipindi Cha julai 2023 hadi Juni 2024 Halmashauri ilipokea Fedha shilingi 19,589,656,444.50 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika Sekta mbalimbali ambapo hadi kufikia Juni 2024 jumla ya shilingi 14,668,636,413.96 zilikuwa zimetumika sawa na asilimia 75%.
Amezitaja Sekta zilizonufaika na fedha hizo ni Sekta ya Afya, Sekta ya Elimu ya awali na Msingi, Sekta ya Elimu Sekondari, Kilimo, Utawala, mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF, pamoja na mfuko wa Jimbo.
Kwa upande wao Madiwani ambao wamepata nafasi ya kuchangia kwa hoja taarifa hiyo kwanza wamepongeza taarifa hiyo ambayo inawatia moyo na kuona Halmashauri imepiga hatua katika suala la ukusanyaji wa mapato ya ndani na hatmaye wakavuka lile Lengo la Mwaka na hivyo wanaomba ziongezwe jitihada katika vile vyanzo vingine vya mapato ambavyo kwa mwaka 2023/24 havikufanya vizuri zaidi basi katika mwaka mpya wa fedha 2024/2025 navyo vikafanye vizuri zaidi.
....@Masasi Dc
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa