Katika kuhakikisha uwekezaji katika sekta elimu unaolenga kuboresha mazingira ya kujifunza na kujifunzia ikiwa ni mojawapo ya njia ya kuinua kiwango cha ufaulu kwa wananfunzi, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kupitia mfuko wa elimu imefanikiwa kutumia milioni 494,500,000 kwa ajili ya kuoresha miundombinu mbalimbali ya shule za msingi na sekondari.
Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari kata ya Chikukwe wakiwa kwenye maandamano wakati wa kilele cha sherehe za Juma la Elimu zilizofanyika leo tarehe 22 juni.2018 katika viwanja vya shule ya masingi Chikukwe
Hayo yamebainishwa na kaimu Afisa Elimu Sekondari ndugu Juma Bushiri wakati akisoma taarifa ya maendeleo ya elimu katika Halimashauri ya Wilaya ya Masasi kwenye kilele cha sherehe za Juma la Elimu zilizofanyika leo tarehe 22 juni,2018 katika viwanja vya shule ya masingi Chikukwe iliyoo kata ya chikukwe na kueleza kuwa Halmashauri imeamua kuwekeza katika elimu ili kupunguza na baadae kuondoa kabisa tatizo la miundombinu ya shule
Kaimu Afisa Elimu Sekondari akisoma taarifa ya maendeleo ya elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wakati wa kilele cha sherehe za Juma la Elimu zilizofanyika leo tarehe 22 juni.2018 katika viwanja vya shule ya masingi Chikukwe
Aidha taarifa hiyo imefafanua kuwa kwa upande wa shule za misingi kupitia mfuko wa elimu, kazi za ujenzi wa matundu ya vyoo 198 na vyumba 21 vya madarasa, nyumba 1, ukarabati wa vyumba 11 vya madarasa, nyumba 1 ya mwalimu na ofisi 1, na umaliziaji wa vyumba 8 vya madarasa na nyumba 3 za walimu zinaendelea kufanyika.
Kwa upande wa shule za sekondari fedha za mfuko wa elimu ujenzi miundombinu ya vyoo matundu 10, vyumba 3 vya madarasa na nyumba 1 ya mwalimu imejengwa, umaliziaji wa vymba 4 vya madarasa na ofisi 1 pamoja na kuingiza umeme katika shule 1 umefanyika.
Makamu Mwnyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya masasi Mhe. leodigar Chilala akikagua (mwenye koti jeusi) banda la wanafunzi wakati wa kilele cha sherehe za Juma la Elimu zilizofanyika leo tarehe 22 juni.2018 katika viwanja vya shule ya masingi Chikukwe
Akihutubia wananchi wa kijiji cha chikukwe katika sherehe za kilele cha Juma la Elimu, mgeni rasmi mhe. Makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Leodigar Chilala amesema kuwa Halmahauri inatekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya maadhimisho ya sherehe hizo inayosema “elimu ni ufunguo wa maisha wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa” kwa kujenga miundombinu na kuajiri walimu wa muda mfupi hasa wa masomo ya sayansi lengo ikiwa ni kuboresha utoaji wa elimu katika shule zetu na hatimaye kuongeza ufaulu.
Makamu Mwnyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya masasi Mhe. Leodigar Chilala (Aliyeshika mike) akihutubia wananchi kwenye kilele cha sherehe za Juma la Elimu zilizofanyika leo tarehe 22 juni.2018 katika viwanja vya shule ya masingi Chikukwe
Mhe. Chilala amewaeleza wazazi na walezi kuwa, kama Halmashauri inawekeza katika miundombinu na kuajiri walimu wa muda kwa masomo ya sayansi, wazazi pia wana wajibu wa kuwekeza katika elimu kwa kuhakikisha watoto wanapata chakula wakiwa shule, kufuatilia maendeleo yao katika masomo pamoja na kuwanunulia vifaa vya shule ili waweze kusoma vizuri.
Kaimu Murugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya masasi Kulwa Maiga (Aliyeshika mike) akitoa neno kwa wananchi kwenye kilele cha sherehe za Juma la Elimu zilizofanyika leo tarehe 22 juni.2018 katika viwanja vya shule ya masingi Chikukwe
Aidha mhe. Chilala amewakumbusha walimu ambao shule zao zilikuwa na matokeo mabaya kwa mwaka 2017 kuweka mikakati mizuri ya kuhakikisha matokea ya mitihani ya mwaka huu 2018 yanakuwa mazuri kwani wakiamua wananweza kupandisha ufaulu. Katika kilele cha sherehe hizo mgeni rasmi ametoa zawadi kwa shule zilizofanya vizuri katika matokeo ya mitihani kwa mwaka 2017 na kwa shule zilizofanya vibaya zimepata vyeti vya himizo.
Mwenyekiti wa kamati ya elimu afya na maji mhe. Edward Mahelela (Aliyeshika mike) akitoa neno kwa wananchi kwenye kilele cha sherehe za Juma la Elimu zilizofanyika leo tarehe 22 juni.2018 katika viwanja vya shule ya masingi Chikukwe kabla ya kufunga sherehe hizo.
Mwalimu wa shule ya sekondari Isidori Shirima akipokea zawadi cheti kwenyekilele cha sherehe za Juma la Elimu zilizofanyika leo tarehe 22 juni.2018 katika viwanja vya shule ya masingi Chikukwe
Mhe. Diwani wa kata ya Chikukwe (Aliyeshika mike) akitoa neno kwa wananchi kwenye kilele cha sherehe za Juma la Elimu zilizofanyika leo tarehe 22 juni.2018 katika viwanja vya shule ya masingi Chikukwe
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa