Katika kuhakikisha wakulima wanapata huduma za ugani kwa uhakika vijijini, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara kwa kutumia fedha za mapato ya ndani imenunua na kuwakabidhi pikipiki maafisa ugani watano ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku kwa ufanisi zaidi zenye thamani ya shilingi milioni 12,500,000.
Maafisa ugani hao kutoka kata za Mbuyuni, Chikunja, Ndanda, Mpindimbi na Chikukwe wamekabidhiwa pikipiki hizo na Afisa kilimo ndugu Kasimu Duwa na kuwaeleza Kuwa pikipiki hizo zitawasaidia kuwafikia wakulima na wafugaji kwa wingi na kwa wakati ili kuleta tija katika kukuza uchumi kupitia kilimo na ufugaji.
Akikabidhi pikipiki hizo Afisa kilimo ndugu Kasimu Duwa kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kwa maafisa ugani hao alisema kuwa Halmashauri imedhamiria kuwawezesha vyombo vya usafiri maafisa ugani wote ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisini kwa kumfikia kila mkulima na mfugaji.
Duwa alitumia nafasi hiyo kuwaasa maafisa ugani hao kutumia pikipiki hizo kwa matumizi sahihi na sio kugeuza bodaboda na ikidhibitika yeyote kufanya hivyo hivyo atachukuliwa sheria ikiwa ni pamoja na kunyang’anywa pikipiki hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya maafisa ugani wenzake, Grace Mpili afisa ugani wa kata ya Mbuyuni alisema kuwa pikipiki hizo zitawasaidia kwa kiasi kikubwa kuwatembela na kutoa huduma kwa wakulima na wafugaji kwa wakati tofauti na awali ambapo ilikuwa ngumu wao kuwafikia wakulima wongi kwa wakati.
Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ina jumla ya kata 34 kati ya hizo kata 25 zina maafisa ugani ambao wamepewa pikipiki bado kata 4 ambazo maafisa ugani wapo na 5 hazina maafisa ugani
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa