Katika kutekeleza kauli mbiu ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati kwa kuanzisha viwanda kila mkoa na halamshauri , Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani mtwara imeanza kutekeleza kwa vitendo Agizo hilo kwa kuwezesha vikundi 42 vya wananwake na vijana vinavyojishughulisha na shughuli za ujasiliamali kwa kutoa mikopo ya riba nafuu katika robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2017/2018.
Akizungumza kabla ya kukabidhiwa hundi za mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 115,545,000/= kwa vikundi hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Changwa M. Mkwazu alisema kuwa ni vema kila kikundi kikafahamu kuwa kina nafasi kubwa ya kuanzisha viwanda vidogoviogo kwani mtaji wa kuanzia wamepata ili waweze kufikia uchumi wa kati kwa kuzalisha bidhaa mbalimbali zenye ushindani katika soko.
Mkwazu alisema kuwa utoaji wa mikopo hiyo kwa vikundi vya wananwake na vijana ni utekelezaji wa agizo za serikali la kutenga asilimia kumi (10%) ya mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi kama njia ya kuimarisha uchumi wa wananchi kupitia shughuli za ujasiliamali.
“Halmashauri imekuwa ikitoa mikopo hii kila mwaka japo kuwa changamoto kubwa ni urejeshwaji wa fedha hizo kwa wakati inayopelekea kutofikia lengo la kuiwezesha jamii kiuchumi kutofikiwa kwa kiwango kikubwa, kwani mikopo inayotolewa inakuwa midogo tofauti na malengo kusudiwa, hivyo niwaase wananvikundi mnaopata mkopo leo mhakikishe mnarejesha kwa wakat ili na wengine waweze kukopeshwa” alisema Mkwazu.
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi Ujenzi na Mazingira Diwani wa kata ya Lukuledi Mhe Victor Antapa waliwatahatharisha wanavikundi kuwa mikopo hiyo imetolewa kisheria na watapaswa kurejesha kwa wakati ili kutoa fursa kwa vikundi vingine kupata mikopo yenye thamani kubwa zaidi na hivyo kuweza kufanya uzalishaji kwa kiwango kikubwa zaidi.
Mhe. Antapa aliwaeleza wanavikundi kuwa kama watafanya shughuli zao kwa uaminifu wanauwezo wa kuanzisha SACCOS ili waweze kutuza fedha zao na hivyo kuongeza mitaji na uzalishaji hatimaye kukuza uchumi wa wanakikundi, jamii na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Hamashauri hiyo Sity Mtalemwa alisema kuwa jumla ya vikundi vya VICOBA endelevu 15 vimefanikiwa kuunganishwa na taasisi za fedha ikiwemo benki ya posta na Mfuko wa wananchi(MEF) na vimekopeshwa jumla ya shilingi Milioni 152,000,000 na idara imeendelea kutoa mafunzo ya ujasilia mali wa VICOBA na vikundi ili kupata uelewa wa mambo mbalimbali ya ujasiliamali.
Mtalemwa alisema vikundi vya wananwake na vijana katika halmashauri ya wilaya ya masasi vimeendelea kufanya vizuri katika masuala ya ujasilia mali ampapo kikundi cha LEMACHI kilichopo ijiji cha Nambawala kimefanikiwa kuwa mshindi wa kwanza katika maonesho ya Ujasiliamali (SIDO) kanda ya kusini ambapo mikoa ya Dar es salaam, morogoro,pwani,lindi na mtwara ilishiriki.
Kwa mwaka 2015/2016 jumla ya shilingi milioni 160,770,000 zilikopeshwa kwa vikundi 95 na kurejeshwa jumla ya shilingi 155,432,150 sawa na asilimia 96% na mwaka 2016/2017 jumla ya shilingi milioni 380,050,000 zilikopeshwa kwa vikundi 102 na zikarejeshwa shilingi 69,379,500 sawa na asilimia 26% .
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa