Halmashauri ya Wilaya ya Masasi leo tarehe 26/06/2025 imemkabidhi Pikipiki mpya aina ya SANLG Bw.Yusuf Sijaona Karume yenye thamani tsh.MIlioni mbili na laki nane (2,800,000/=) ikiwa ni gharama za kulipwa fidia ya Madhara aliyoyapata baada ya Kugongwa na gari la Serikali la Halmashauri hiyo.
Bw. Yusuf Sijaona ambaye alifungua shauri Mahakama kuu ya Mtwara mnamo mwaka 2020 kuidai Halmashauri ya Wilaya ya Masasi tshs milioni 100 ikiwa ni gharama zake baada ya kusababishiwa madhara.
Hata hivyo baada ya majadiliano Halmashauri na Mdai walikubaliana kumlipa shilingi milioni 10 na kupewa Pikipiki mpya, hivyo Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imefanikiwa kununua pikipiki mpya na tayari leo hii juni 26, 2025 imemkabidhi Bw.Yusuf Sijaona Karume na hii ni baada ya kumaliza kumlipa shilingi milioni 10.
Makabidhiano ya Pikipiki hiyo yamefanyika katika viunga vya Halmashauri ya zamani ya Masasi mjini huku Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Ndg.Optatus Lusolela ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu amekabidhi Pikipiki hiyo kwaniaba ya Mkurugenzi Mtendaji.
Kwaupande wake Bw.Yusuf mara baada ya kuipokea Pikipiki hiyo amemshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kwa kufanikisha suala hilo ambalo limefuta machozi kwake.
26/06/2025.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa